ABIRIA 48 WA PRECISION AIR WANUSURIKA MWANZA
http://melckstudio.blogspot.com/2014/07/abiria-48-wa-precision-air-wanusurika.html

- Ndege hiyo ilikuwa ikiruka kwenda Nairobi nchini Kenya kupitia Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro.
Mwanza. Ndege
ya Shirika la PrecisionAir iliyokuwa imeruka kwa safari zake kutoka
Mwanza kwenda Nairobi nchini Kenya kupitia Kilimanjaro jana, imelazimika
kutua kwa dharura baada ya kupata hitilafu ikiwa angani.
Taarifa
zilizopatikana kutoka kwa baadhi ya abiria waliokuwamo ndani ya ndege
hiyo namba 5H-PWC ATR 72, zilieleza kuwa tayari walikuwa wameruka lakini
baada ya muda mfupi waliambiwa hawawezi kuendelea na safari kutokana na
ndege kupata hitilafu.
Baada
ya kuruka, ndege ilitaka kukunja magurudumu kwa ndani ikashindikana hali
iliyomlazimisha rubani kuzunguka eneo la uwanja huo, huku akijaribu
kuyarudisha bila mafanikio na kuamua kutua kwa dharura.
Alisema abiria 48 waliokuwa kwenye ndege hiyo hadi jana saa 12:00 jioni walikuwa wanasubiri nyingine ili kuendelea na safari.
Akizungumza
kwa simu Meneja wa Uwanja wa Ndege wa Mwanza, Ester Madale alisema
hitilafu hiyo ilikuwa ya kawaida hivyo haikuwa na madhara.
Madale
alisema iliruka saa 7:54 mchana kwenda Kilimanjaro, lakini baada ya
kuruka magurudumu yalishindwa kujikunja kurudi ndani hivyo rubani
alijaribu kuyarudisha ikashindikana, hivyo akalazimika kutua kwa
dharura.
“Hitilafu
hiyo ni ya kawaida, wahandisi wetu waliangalia hitilafu hiyo na saa
9:15 alasiri walifanya majaribio kuirusha na imetua, hivyo siyo tatizo
kubwa la kawaida,” alisema Madale.
Matukio ya karibuni
Desemba
13, mwaka jana ndege ya PrecisionAir aina ya ATR 42-600 ilipasuka
magurudumu manne ya nyuma wakati ikitua uwanja wa KIA, miongoni mwa
abiria waliokuwa ni Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa.
Julai 24, 2012 ndege ya shirika la PrecisionAir magurudumu yalipasuka wakati ikitua Uwanja wa Ndege mkoani Kigoma.
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapowekwa kwenye mtandao huu.BOFYA HAPA