ALIPWA MAMILIONI YA PESA KAMA FIDIA YA KIFO CHA MUMEWE KUTOKANA NA UVUTAJI WA SIGARA
http://melckstudio.blogspot.com/2014/07/alipwa-mamilioni-ya-pesa-kama-fidia-ya.html
Kampuni
ya upili kwa ukubwa katika utengenezaji wa sigara nchini Marekani
imeagizwa kulipa kitita kikubwa cha dola billioni 23 kwa mke wa
mwathiriwa mmoja wa sigara aliyefariki kutokana na saratani ya mapafu.
Kwa
mujibu wa shirika la habari la BBC, Mjane huyo Cynthia Robinson
alichukua hatua dhidi ya kampuni ya sigara ya R.J Reynolds baada ya kifo
cha mumewe aliyekuwa na miaka 36.
Kampuni hiyo imeyataja malipo hayo kama yasio na haki na kusema kuwa itakata rufaa.
Wakili
wa bi Robinson amesema kuwa kampuni hiyo ya sigara iliuza sigara hizo
bila kutoa tahadhari yoyote kuhusu tishio la uvutaji wake.kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapowekwa kwenye mtandao huu.LIKE HAPA