ALIYEMNG’ATA HAUSIGELI NA KUMCHOMA PASI AACHIWA KWA DHAMANA

Amina Said Maige (mwenye miwani) akisubiria kupandishwa kizimbani.Amina akiwa chini ya ulinzi akisubiri kupanda kizimbani....akijiziba kwa aibu kabla ya kupanda kizimbani.Wanaharakati wakiwa nje ya Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni wakifuatilia kesi hiyo.Wanaharakati wakisubiri kwa hamu kusomwa kwa kesi ya Amina dhidi ya hausigeli wake, Yusta.
YULE mwanamke anayejulikana kwa jina la Amina Said Maige ambaye anakesi ya kumng’ata na kumchoma kwa pasi hausigeli wake, Yusta  Kashinda (20), ameachiwa kwa dhamana.
Amina alisomewa mashtaka na Wakili wa Serikali, Mohamed Salum mbele ya Hakimu Mkazi, Yohana Yongolo.
Mahakama imemuachi kwa dhamana baada ya masharti yake ya kuwapata waajiriwa wawili pamoja na kiasi cha shilingi milioni tatu kila mmoja kukamilika.

Amina alikamatwa Juni 4 mwaka huu na kufikishwa Kituo cha Polisi Oysterbay kwa kupatikana na kosa la Kumng’ata, kumchoma kwa pasi na kumpiga mwili mzima, Yusta. Kesi yake ipo katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni, Dar ambapo mara ya kwanza alisomewa mashtaka Juni 12 na kesi kuhairishwa mpaka Juni 26 pamoja na Julai 10.
Kesi yake itasomwa tena Julai 22 mwaka huu.
(PICHA / HABARI: DEOGRATIUS MONGELA / GPL)
 kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapowekwa kwenye mtandao huu.BOFYA HAPA

Related

KITAIFA 6248025240075280706

Asia - Leo

MZIWANDA - MSONDO NGOMA

TONBOY

TONBOY

CONTACT

Melck Studio
Tel : +25578920034
+255757605268
E-mail : melckstudio@gmail.com

SHOW LOVE TO THIS

Hot in week

Recent

Comments

Visitors


web stats
item