BREAKING NEWZ: BOKO HARAMU WASHAMBULIA TENA
http://melckstudio.blogspot.com/2014/07/breaking-newz-boko-haramu-washambulia.html

Watu
kadhaa katika mji wa Dille, Kaskazini mashariki mwa Nigeria, wameuawa,
na wengine kutorokea vijiji jirani baada ya kushambuliwa na watu
wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa Boko Haram.
Aidha, nyumba kadhaa zilichomwa katika shambulizi hilo lililotekelezwa siku ya Jumatatu
Anavyoripoti Raliya Zubairu kutoka Abuja, viongozi nchini Nigeria wamedhibitisha shambulizi hilo, lakini hawajatoa usemi ni watu wangapi waliuawa.Inasemekana kuwa raia walidhani kuwa shambulizi hilo lilitekelezwa na wanajeshi ili kukabiliana na wanamgambo wa Boko Haram bali sivyo.
Hata hivyo wanapeleleza madai ya raia kuwa walishambuliwa na ndege za wanajeshi.
Shahidi
aliyezungumza na BBC alisema watu 25 waliuwawa, huku wanamgambo 20
wakiuawa na wakaazi wanaoshika doria katika eneo hilo.
Hayo
yakijiri, wanaharakati wa haki za kibinadamu wametoa ripoti hii leo
inayosema kuwa takriban watu elfu mbili wameuwawa na wanajeshi tangu
mwanzoni mwa huu mwaka.
>>BBC
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapowekwa kwenye mtandao huu.LIKE HAPA