JAMES RODRIGUEZ ATUA REAL MADRID AWA MCHEZAJI WA 4 GHALI DUNIANI
http://melckstudio.blogspot.com/2014/07/james-rodriguez-atua-real-madrid-awa.html

Mshambulizi
wa Colombia na Monaco James Rodriguez amezunduliwa kama mchezaji wa
Real Madrid baada ya kutia sahihi mkataba wa miaka 6 na mabingwa hao wa
bara Ulaya.
Mchezaji
huyo wa aliyetwaa taji la mfungaji mabao mengi katika kombe la dunia
huko Brazil amesaini mkataba wa miaka 6 na klabu hiyo.
james huenda James akapokea kitita cha dola milioni mia moja.
Kutua kwake huko Bernabeu kumemuweka Rodriguez katika mizani sawa na Gareth Bale, Cristiano Ronaldo na Luis Suarez.

Iwapo
Rodriguez atalipwa takriban pauni millioni 80 basi huenda atakuwa
mchezaji wa nne ghali zaidi nyuma ya Bale, Ronaldo na Suarez.
Rodriguez
aligonga vichwa vya habari baada ya kutinga mabao 6 licha ya timu yake
ya Colombia kubanduliwa nje ya kombe la dunia katika hatua ya robo
fainali.
Rodriguez
alifunga mabao dhidi ya Ugiriki , Ivory Coast na Japan lakini
atakumbukwa zaidi kwa bao lililopigiwa upatu kuwa bora zaidi katika
mashindano hayo dhidi ya Uruguay.
Kabla
ya kujiunga na Monaco Rodriguez alikuwa amedhihirisha udeddea wake huko
Ureno alikotwaa mataji matatu ya ligi akiwa na klabu ya Porto.

Naibu
mwenyekiti wa wa klabu ya Monaco Vadim Vasilyev alisewaambia wanahabari
kuwa klabu hiyo haikuwa na niya ya kumuuza mshambulizi huyo lakini
hawakutaka kupitwa na kitita kikubwa kilichotolewa kwao na kumweka
katika mizani sawa na washambulizi ghali zaidi katika hstoria ya
kandanda.
Madrid ilitoa kitita cha pauni milioni 80 kumnunua Ronaldo alipotokea Manchester United mwaka wa 2009.
Na
ulimwengu na kandanda ulipodhania kuwa historia hiyo haingevunjwa Madrid
ilitoa pauni milioni 85.3m mwaka uliopita na kumnunua Bale kutoka kwa
Tottenham ya Uingereza.
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapowekwa kwenye mtandao huu.LIKE HAPA