KAMANDA KOVA ATOBOA SIRI YA BENKI NYINGI KUVAMIWA NA MAJAMBAZI HAPA NCHINI
http://melckstudio.blogspot.com/2014/07/kamanda-kova-atoboa-siri-ya-benki.html
JESHI
la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limefichua siri ya kuongezeka
kwa vitendo vya ujambazi katika Benki mbalimbali hapa nchini na kusema
vitendo hivyo vinasababishwa na wamiliki wa benki hizo kulipuuza jeshi
la polisi pale linapowapa ushauri.
![]() |
Kamishina
wa polisi kanda maalum ya Daresalaam Suleimani Kova akitoa ufafanuzi
jambo kwenye mkutano na waandishi wa Habari Jijin Dar es Salaam.
Kauli
hiyo ya jeshi la polisi Kanda ya Dar es Salaam imekuja ikiwa ni siku
moja kupita baada ya watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi kuvamia katika
Benki ya Stanbic tawi la Kariakoo lililoko mtaa wa Swahili na kukomba
mamilioni ya pesa aliyokuwa nayo mteja.
Kauli
hiyo imetolewa muda mfupi uliopita na kamishna wa polisi kanda maalum
ya Dar es Salaam,Suleiman Kova wakati wa mkutano na waandishi wa habari
jijini Dar es Salaam,ambapo alisema watu wanaochangia vitendo hivyo vya
ujambazi kuzidi kuongezeka katika benki mbalimbali hapa nchini ni
wamiliki wa benki kupuuza ushauri wa jeshi la polisi.
Ushauri
wa jeshi la polisi ni ule uliowataka waache kutumia walinzi wa
makampuni binafsi peke yake hivyo watumie na walinzi kutoka jeshi la
polisi.
“Nataka
niwambie waandishi hivi vitendo vya uvamizi kwenye mabenki vinatokana
na wamiliki wa mabenki hayo kupuuza ushauri wetu uliowataka kwenye
shughuli za ulinzi kwenye mabenki watumike polisi tu,lakini wao
wakapuuza,ukitaka kuamini nenda kwenye mabenki yanayolindwa na polisi
kama utaona kama kuna uvamizi wowote unaotokea,kwa sababu majambazi hao
wanashindwa kuvamia kutokana na umakini wa jeshi la polisi”alisema Kova
Kamishna
Kova,alisema kwa sasa jeshi la polisi limejipanga kuongea na Benki kuu
ya Tanzania (BOT) ambaye ni kiongozi wa benki zote hapa nchini na
kutafuta ufumbuzi wa tatizo hili la benki zingine kupuuza ushauri huo wa jeshi la polisi.
Aliongeza
kuwa jeshi hilo la polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam, limeanza msako
mkali wa kuwatafuta majambazi watano waliovamia jana majira ya mchana kwenye Benki ya Stabinc Tawi la Kariakoo lililoko mtaa wa Shwahili .
Kwa Mujibu wa Kamishna Kova alisema watu watatu kati yao waliingia
ndani ya benki hiyo wakiwa na mifuko mikubwa wakijifanya ni wateja
wanapeleka fedha nyingi katika benki hiyo, na watu hao walipoingia ndani
walianza kuwalazimisha kuvuka wigo wateja wa kwaida na kutaka kuingia
kwa nguvu kupora fedha.
Lakini
kutokana na benki hiyo ya Stabinc kuwa na mitambo ya aina mbalimbali
ikiwa ni pamoja na ving'ora vya tahadhari,ikasaidia kwa majambazi hao
kushindwa kuingia ndani kuiba pesa za benki hiyo kutokana na ving'ora
hivyo kupiga kelele na kuanza kuwapa uwoga majambazi hao ,ambapo
walifanikiwa kuiba pesa za mteja mmoja ambaye alikuwa anataka kuweka
pesa kwenye benki hiyo.
Kova
alisema majambazi hao walipotoka nje ya benki hiyo walipiga risasi juu
ili kuwapa hofu wananchi waliokuwa nje ya benki hiyo,ambapo kwa mujibu
wa kamishna Kova anasema bado wanaendelea kuwafuatilia majambazi hao.
Katika
hatua nyingine jeshi hilo la polisi limejipanga ipasavyo kwenye sikukuu
ya IDD El Fitr 2014,ambapo jeshi hilo limesema limepanga kushikirikiana
na vyombo mbalimbali vya ulinzi na Usalama ikiwa ni pamoja na
kikosi cha zima moto na uokoaji,kampuni binafsi za ulinzi lengo ni
kuhakikisha wananchi wanafurahia kwa utulivu na amani kwenye sikukuu
hii.
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapowekwa kwenye mtandao huu.LIKE HAPA
|