LIVERPOOL YAMSAJILI MARKOVIC KWA PAUNDI MIL 20, ASHLEY COLE ATIMKIA ITALY

Wednesday, July 16, 2014

Liverpool imetumia £20m kumsajili Markovic
Pauni millioni 20 ndicho kima imekitumia Liverpool kumhamisha Lazar Markovic kutoka Benfica.
Mserbia huyo aliiwezesha Benfica kutwaa taji la Ureno msimu uliopita na anasema anamatumaini makubwa ya kuwaridhisha mashabiki na mwenye club hiyo.
Maneno hayo ya busara yanahitajika sana huko Liverpool baada ya nyota wao Suarez kufifizwa na kashfa ya kung'ata wachezaji wenzake hasa katika mhadhara wa jukwaa la kombe la dunia.

Hata hivyo hilo halijashukisha dau la Suarez sanaa kwani Liverpool waatavuna £75m kutoka Barcelona ambako Suarez sasa amepata makao mapya.
Hivyo ili kujiimarisha kwa kampeni yao ya msimu unaokuja wa Champions League na Premier League walioambulia nafasi ya pili kinyume na matarajio ya wengi, Markovich mwenye umri wa miaka 20 anakuwa mchezaji wa nne kupata mkataba na Liverpool hivi karibuni.
Je Liverpool itatumia pesa ngapi kumsajili mshambuliaji chipukizi Origi
Wengineo ni Mshambuliaji Rickie Lambert, 32 kwa pauni £4m na Adam Lallana, mwenye umri wa miaka 26, kwa pauni £25m, wote walitokea Southampton.
Kumbuka Liverpool pia inasubiri uamuzi wa Divock Origi, mwenye asili ya Kenya , aliyatamba kweli katika safu ya ushambuliaji akiwa kombe la dunia na timu yake ya Ubeleji.
Kweye umri wa miaka 19 pekee wengi wanasubiri kwa hamu kuona Je Liverpool itatumia pesa ngapi kumpata Origi. 

Je Waingereza waogopa vilabu vya nje?


Mlinzi wa zamani wa Arsenal na Chelsea, Cole aelekea klabu ya Roma Uitaliano
'Waingereza hawapanii kuchezea vilabu vya nje'- asema Ashley Cole
Mlinzi huyo wa zamani wa Arsenal na Chelsea, mwenye umri wa miaka 33, amesema kuwa wanasoka wa Uingereza wanaogopa kujisajili katika vilabu vya nje ya Uingerea - kwanini ?
Adai wanahisi wametulia tuliii nyumbani hivyo hawataki au hawawezi bughdha za vilabu vya ugenini.
Yeye mwenyewe Ashley, anahamia Roma Uitaliano wakati mkaba wake na Chelsea unapokamilika.
   

kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapowekwa kwenye mtandao huu.LIKE HAPA

Related

MICHEZO 2588500660431871072

Asia - Leo

MZIWANDA - MSONDO NGOMA

TONBOY

TONBOY

CONTACT

Melck Studio
Tel : +25578920034
+255757605268
E-mail : melckstudio@gmail.com

SHOW LOVE TO THIS

Hot in week

Recent

Comments

Visitors


web stats
item