MFANYAKAZI WA NDANI ABAKWA HADI KUFA HUKO DODOMA,ALIPOTEA TANGU JUMAMOSI ILIYOPITA
http://melckstudio.blogspot.com/2014/07/mfanyakazi-wa-ndani-abakwa-hadi-kufa.html

Kinamama
walio karibu na familia ya marehemu Isabela Andrew aliyebakwa hadi kufa
wakiangua kilio baada ya kushuhudia mahali mwili wake ulipokutwa huko
Area C mjini Dodoma jana.
Mfanyakazi
wa ndani, Isabella Andrew (18), amefariki dunia na kifo chake kikidaiwa
kusababishwa na kubakwa na watu wasiojulikana.
Mwili
wa msichana huyo ulikutwa ukiwa umeharibika katika moja ya pagale,
lililopo Area C, Dodoma Mjini na mwandishi wetu alishuhudia ukitolewa
hapo kwa machela huku polisi wakiwahoji mashuhuda wa tukio hilo.
Mkazi
wa Mtaa wa Kiwanja cha Ndege, Jackson Coy aliyekuwa akiishi na binti
huyo alisema msichana huyo alipotea tangu Jumamosi iliyopita.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Dodoma, David Misime, alisema mwili huo uliokotwa
jana saa mbili asubuhi na kwamba polisi wanaendelea na uchunguzi kubaini
chanzo cha kifo chake.
Mwili
huo ulibainika baada ya mama mmoja, Rehema Msambile kufika katika
pagale hilo alipokuwa akifuatilia nyendo za mtoto wake ambaye juzi
alipigwa kwa tabia ya utoro shuleni.
“Niliamua
leo (jana) kumfuatilia, nikaanza katika mapagale.Nilipofika hapa ndipo
nikaona mwili wa marehemu ikabidi nimuite jirani hapo aje aone,”
alisema.
Diwani
wa Kata ya Kiwanja cha Ndege, Henry Kandenga alisema mazingira
yanaonyesha kuwa binti huyo alibakwa kwa sababu walikuta nguo za ndani
zikiwa pembeni.
“Hakuna
yowe iliyosikika kwamba kuna mtu anauawa ukizingatia kwamba nyumba ziko
jirani na hata nyumba aliyokuwa akiishi ni jirani na mahali
alipokutwa,” alisema
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Dodoma.kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapowekwa kwenye mtandao huu.LIKE HAPA