Msikiti wa Mashia wateketezwa moto Istanbul, Uturuki
http://melckstudio.blogspot.com/2014/07/msikiti-wa-mashia-wateketezwa-moto.html

Katibu Mkuu wa zamani wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC amesikitishwa na kulaani kitendo cha kushambuliwa na kuteketezwa moto msikiti wa Waislamu wa madhehebu ya Shia mjini Istanbul, nchini Uturuki. Ekmeleddin Ihsanoglu amesema kuwa, kitendo cha kuchoma moto eneo la ibada na hasa msikiti, ni cha kinyama na hakipaswi kunyamaziwa kimya.
Katibu Mkuu wa zamani wa OIC ametahadharisha juu ya njama za kutaka kuwagombanisha Waislamu wa madhehebu ya Shia na Suni nchini Uturuki na kusisitiza kwamba, Waislamu nchini Uturuki wanapaswa kuwa macho na njama hizo za maadui wa dini tukufu ya Kiislamu.
Ekmeleddin Ihsanoglu ambaye ametangaza kwamba atashiriki kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi wa rais nchini Uturuki, amesisitiza juu ya kutiwa mbaroni na kufunguliwa mashtaka wale wote waliohusika na shambulio hilo.
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapowekwa kwenye mtandao huu.BOFYA HAPA