MTU MMOJA AFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI WILAYANI MOMBA
http://melckstudio.blogspot.com/2014/07/mtu-mmoja-afariki-dunia-papo-hapo-baada.html
MTU
MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA BAKARI DAMSON (27) MKAZI WA MAJENGO
AMEFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI LENYE NAMBA ZA
USAJILI ADC 3671 AINA YA TOYOTA LAND CRUISER LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA
DEREVA FRANK MATHEW SIKONGA (29) MKAZI WA CHIPAKA.TUKIO
HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 15.07.2014 MAJIRA YA SAA 22:00 USIKU HUKO
KATIKA MTAA WA MWAKA, KATA NA TARAFA YA TUNDUMA, WILAYA YA MOMBA, MKOA
WA MBEYA. CHANZO CHA AJALI BADO KINACHUNGUZWA. MWILI WA MAREHEMU
UMEHIFADHIWA KITUO CHA AFYA TUNDUMA. DEREVA AMEKAMATWA KWA HATUA ZAIDI
ZA KISHERIA.
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL N. MASAKI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO HASA KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
Imetolewa na:
[BARAKAEL N. MASAKI – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapowekwa kwenye mtandao huu.LIKE HAPA