MUME AMVIZIA MKEWE AKISWALI AMPIGA HADI KUZIMIA
http://melckstudio.blogspot.com/2014/07/mume-amvizia-mkewe-akiswali-ampiga-hadi.html
Bi. Nasra Dafa (30) aliyeshambuliwa na mume wake wakati akiswali.
TUHUMA nzito
ya aina yake ambayo haijawahi kutokea ambapo mkazi mmoja wa Tandale –
Kwatumbo wilayani Kinondoni jijini, Idd Mpenda anadaiwa kumshambulia na
kumjeruhi hadi kuzimia mkewe, Nasra Dafa (30) wakati
akiswali.Akizungumza na Amani huku akimwaga machozi, mwanamke huyo
alisema tukio hilo lilijiri Julai 28, mwaka huu saa saba mchana wakati
akiswali maeneo ya duka lake lililopo Tandale.
ILIKUWA KUSHTUKIZA
Alidai
kwamba alikuwa katika kusujudu, mara mumewe alitokea na kumshambulia
kwa mateke, ngumi na viatu kisha akamburuza chini hadi nje hali
iliyosababisha nguo aliyovaa kuvuka na kubaki kama alivyozaliwa!“Kama
unavyoniona, nimeumia sehemu mbalimbali za mwili. Kiatu ndiyo
kimeniumiza sana.
ATINGA KITUO CHA POLISI
Alisema
baada ya tukio hilo kutokea alijivuta na kuvaa gauni lingine kisha
akakimbilia Kituo Kidogo cha Polisi Tandale ambapo polisi walimwambia
ishu yake ni nzito na kumtaka aende Kituo cha Polisi Magomeni (vyote
vipo Dar).
ASIMULIA VIPIGO, UKE WENZA
Mwanamke
huyo aliweka hadharani kwamba mumewe amekuwa akimpiga mara kwa mara na
tatizo kubwa ni uke wenza ambapo alidai ameoa mke wa pili hivi karibuni
na mapenzi baina yao yamezorota.
“Mimi kabla
ya kufunga naye ndoa Januari Mosi, 2013 mume wangu alikuwa na mke
mwingine lakini aliamua kumpa talaka baada ya kumweleza kuwa mimi sitaki
kuwa mke mwenza.
“Tukawa tunaishi naye lakini hata hivyo hakuchukua muda mgogoro ukaanza ndani ya nyumba.
SAKATA LAFIKA KWA NDUGU
Mwanamke
huyo aliendelea kusema kwamba hali ilizidi kuwa mbaya hadi ikafika kwa
wana ndugu kwa suluhu, walipatanishwa lakini baada ya muda mgogoro
ukaendelea na kuna siku mumewe akamwambia ameoa mke mwingine wiki tatu
nyuma.
SIKU YA TUKIO
“Siku ya
tukio, nilikuwa naswali. Unajua wakati wa Mfungo wa Ramadhani lazima
Muislam kuswali kwa kuzingatia taratibu zote za dini. Basi, alikuja na
kuniita nitoke nje lakini sikutoka.“Niliona nimalize kwanza kuswali
ndipo nitoke, lakini kabla sijamaliza akaja na kunishambulia kama
niliovyokwambia kisha akachukua funguo na kufunga duka.
“Alipotoka
hapo akaenda kwenye duka lingine la kuuza vocha nalo akalifunga na
kuchukua fedha zote na kuondoka nazo huku muuzaji akiambiwa aende
kwake,” alisema mwanamke huyo.
Amani
lilifika kwenye Kituo cha Polisi Magomeni na kuambiwa na askari mmoja
kuwa taarifa hizo zipo na mtuhumiwa anashikiliwa hapo, lakini akashauri
atafutwe Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, ACP Camilius Wambura kwa
maelezo zaidi. Kamanda huyo hakupatikana ofisini kwake hadi tunakwenda
mtamboni.
SHEHE MKUU ASAKWA
Shehe
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Musa Salum hakupatikana kuzungumzia
makosa ya mume wa Kiislamu kumpiga mkewe wakati akiswali ndani ya Mwezi
Mtukufu.Hata hivyo, Maalim Hassan Yahya Hussein wa Magomeni Mwembechai
alipoulizwa alisema Uislamu haujatoa ruhusa kwa mwanaume kumpiga mkewe
wakati anaswali hata kama amefanya kosa kubwa kiasi gani.
“Uislamu
haujaruhusu kwa hali yoyote udhalilishaji na kuna hadithi zinazokataza
mtu kumdhuru mwenzake. Kuna masharti sita yamewekwa kabla ya mume
kufikia hatua ya kumwadabisha mkewe,” alisema Maalim Hassan.Akaendelea:
“Kabla mume hajampa adhabu mke anapaswa kwanza kumpa nasaha kwa kosa
alilotenda na sharti la pili ni kumpa mawaidha ama yeye mwenyewe au
atafute mtu.
“Sharti
la tatu ni kumkumbusha mara kwa mara na sharti la nne ni kumhama
malazi, yaani kumuacha alale peke yake. Sharti la tano, akikosa ni
kwenda kushitaki kwa wazee au katika vyombo vya sheria ikiwemo kwa kadhi
na viongozi wa dini.“Sita ndiyo kumpiga, lakini kipigo ambacho
hakitamdhuru kwani hutakiwi kumpiga ukiwa na hasira.
Credit GPL
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapowekwa kwenye mtandao huu.LIKE HAPA