NDEGE YA ALGERIA ILIYOKUWA NA WATU 116 YAANGUKA
http://melckstudio.blogspot.com/2014/07/ndege-ya-algeria-iliyokuwa-na-watu-116.html
Ndege ya shirika la Air Algeria iliyokuwa ikitokea nchini Burkina faso
kwenda Algies na kuripotiwa kupotea kwenye radar mapema leo,
Imethibitishwa kuwa imeanguka.Msako wa kutafuta mabaki ya ndege hiyo unaendelea na ilikuwa na abiria zaidi ya 100 na wafanyakazi 6.
Awali mamlaka inayohusika na uchunguzi wa anga ilisema ilipoteza mawasiliano na ndege hiyo saa 0155 GMT, au dakika 55 50 baada ya ndege kupaa. Hiyo ina maana kuwa ndege hiyo imepotea kwa saa kadha kabla ya habari hiyo kujulikana.
Ndege hiyo ilikuwa ikitoka Ouagagougou, Mji mkuu wa Burkina faso kwenda nchini Algeria.
Mwezi Februari ndege ya kijeshi ya Algeria ilianguka na kuuwa watu 77 waliokuwemo.
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapowekwa kwenye mtandao huu.LIKE HAPA
