PIGO BRAZIL: NAYMAR AVUNJIKA MFUPA, HATAENDELEA NA MICHUANO YA KOMBE LA DUNIA
http://melckstudio.blogspot.com/2014/07/pigo-brazil-naymar-avunjika-mfupa.html

Staa huyo mwenye mabao manne mpaka sasa kwenye michuano hiyo, alitolewa uwanjani dakika tatu kabla ya mechi yao dhidi ya Colombia kumalizika.
Katika mechi hiyo, Brazil walishinda mabao 2-1 na kutinga Nusu Fainali ambapo watakutana na Ujerumani Julai 8 mwaka huu.
Kwa mujibu wa taarifa za daktari wa timu ya Brazil, Neymar atakaa nje kwa takribani wiki nne.