http://melckstudio.blogspot.com/2014/07/rais-kagame-azungumzia-uhusiano-kati-ya.html
Rais Kagame azungumzia uhusiano kati ya Rwanda na Tanzania
Rais
wa Rwanda Paul Kagame amesema kwamba Rwanda na Tanzania ni mataifa
ndugu na yataendelea kuwa ndugu kwa sababu yanachangia udugu huo.
Rais Paul Kagame ameyasema hayo mjini Kigali kwenye kikao na waandishi
wa habari.Nchi za Rwanda na Tanzania zilikabiliwa na wakati mgumu
kuanzia mwaka jana kutokana na kutofautiana kuhusu kundi la waasi wa
kihutu la FDLR linaloendesha mambo yake mashariki mwa Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo dhidi ya utawala mjini Kigali.