TAARIFA KAMILI JUU YA NDEGE YA MALAYSIA NYINGINE ILIYOPOTEZA MAISHA YA WATU 295 JANA YADAIWA ILISHAMBULIWA
http://melckstudio.blogspot.com/2014/07/taarifa-kamili-juu-ya-ndege-ya-malaysia.html

Ndege hii ilikuwa inatoka Amsterdam kuelekea Kualar Lumpur
Maafisa nchini Ukraine wanasema
kuwa ndege ya abiria iliyoanguka nchini humo ilidunguliwa katika eneo la
mashariki mwa taifa hilo ambako waasi wanaoiunga mkono Urusi wamekuwa
wakipigana na vikosi vya serikali.
Wanasema abiria wote 298 waliokuwa katika ndege
hiyo ya shirika la Malaysia iliyokuwa ikisafiri kutoka Amsterdam
kuelekea Kualar Lumpur wamefariki.Rais wa Ukraine Petro Poroshenko alitaja tukio hilo kama kitendo cha ugaidi.
Maafisa wa Ukraine walichapisha kile walichotaja kuwa mawasiliano ya simu yaliyonaswa kati ya waasi wakiwaeleza maafisa wa Urusi kwamba ni wao ndio waliohusika katika kuindungua ndege hiyo.
Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Ukraine, Pavlo Klimkin, amesema kuwa serikali ina ushahidi wa kutosha kwamba ndege hiyo ilidunguliwa.
'Je waasi walihusika?'
'Tulinasa pia mawasiliano ya simu kati ya magaidi hao wakizungumzia kundunguliwa kwa ndege hiyo.Kwa sasa tunatafsiri sauti zao na kisha tutaziweka kwenye mtandao wa internet ili kuthibitisha hilo."

Mabaki ya ndege ya Malaysia iliyodunguliwa
Kadhalika marekani imesema kuwa inaamini ndege hiyo ililipuliwa angani na wala halikuwa tukio la ajali.
Makamu wa rais Joe Biden hata hivyo amesisitiza kuwa Marekani bado inatafuta maelezo.
''Ndege ya Malaysia iliyokuwa ikitoka Ulaya magharibi kuelekea Kuala Lumpur, yaelekea ilipokuwa ikivuka karibu na mpaka kati ya Ukraine na Urusi, nasema yaelekea kwa sababu hatuna taarifa za kina, nataka kuwa makini na kile ninachosema yaelekea ilidunguliwa, ilidunguliwa na wala sio ajali. Ililipuliwa kutoka angani. Tunaona ripoti kwamba huenda raia wa Marekani walikuwa kwenye ndege hiyo na bila shaka huo ndio wasiwasi wetu wa kwanza.''
Rais wa Urusi, Vladimir Putin, amesema kuwa Ukraine inapaswa kuwajibika katika tukio la udunguaji wa ndege hiyo.
Msemaji wa serikali ya Urusi amesema kuwa mkasa huo haungetokea ikiwa Kiev haingeimarisha harakati zake za kijeshi mashariki mwa Ukraine.
Chanzo bbcswahili
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapowekwa kwenye mtandao huu. LIKE HAPA