TUFANI LENYE NGUVU LAELEKEA JAPAN


Maelfu ya watu wametakiwa kutafuta hifadhi salama wakati tufani lenye nguvu likipita katika kisiwa cha Okinawa nchini Japan.
Tufani hilo lililopewa jina la Neoguri lilotarajiwa kukatisha katika kisiwa cha Okinawa siku ya Jumanne, likiandamana na upepo mkali na mvua kubwa.
Safari za ndege zimefutwa na shule kufungwa. Kituo cha TV cha huko kimeonesha picha za miti ya michikichi ikirushwa na upepo mkali unaovuma.
Watabiri wa hali ya hewa wanasema tufani hilo huenda likawa miongoni mwa kubwa zaidi kuwahi kuonekana Japan, likisababisha mawimbi yenye urefu wa hadi mita 14.
Mamlaka za huko zimewataka wakazi wake wapatao 480,000 kukaa ndani ya nyumba zao au kwenda katika vituo vya kijamii kutafuta hifadhi.
Zaidi ya nyumba 50,000 zimeripotiwa kuwa bila ya umeme na kituo kimoja cha kusafisha mafuta kimesimamisha shughuli zake.
Tufani Neogori limeripotiwa kuonekana likielekea upande wa kaskazini kwa kasi ya kilomita 25 kwa saa likiwa na upepo unaovuma kwa kasi ya hadi kilomita 252 kwa saa, limeripoti shirika la habari la Kyodo.

Related

MATUKIO 5736783210725000410

Asia - Leo

MZIWANDA - MSONDO NGOMA

TONBOY

TONBOY

CONTACT

Melck Studio
Tel : +25578920034
+255757605268
E-mail : melckstudio@gmail.com

SHOW LOVE TO THIS

Hot in week

Recent

Comments

Visitors


web stats
item