UINGEREZA KUJADILI MUSWADA WA KUJIUA
http://melckstudio.blogspot.com/2014/07/uingereza-kujadili-muswada-wa-kujiua.html

Askofu
mkuu wa zamani wa Cantebury Lord Carey amesema kuwa ataunga mkono
sheria ambazo zitahalalisha watu wanaougua kupitia kiasi nchini
Uingereza na Wales kupata usaidizi wa kujiua.
Katika
taarifa yake ndani ya gazeti la Daily Mail Lord Carey ameondoa
pingamizi yake dhidi ya mswada huo kufuatia hali inayowakumba watu
wanaougua.
Wabunge
wataujadili mswada huo siku ya ijumaa.Lakini Askofu mkuu wa Cantebury
anayehudumu kwa sasa Justin Welby ameutaja mswada huo kama ulio na
makosa na hatari kubwa.
Mswada
huo uliowasilishwa na mbunge wa chama cha leba Lord Falconer utawapa
fursa watu wazima nchini Uingereza na Wales kupata usaidizi wa kujitoa
uhai.
Fursa hiyo itashirikisha wale walio na chini ya miezi sita kuishi.
Madaktari
wawili watalazimika kuthibitisha iwapo mgonjwa anaugua kupitia kiasi na
kwamba wameafikia uamuzi wao wenyewe wa kujitoa uhai.
Takriban wabunge 110 wameorodheshwa kuzungumza wakati bunge litakapojadili mswada wa wanachama binafsi siku ya ijumaa.

Lord Carey
Wakati
Askofu Lord Carey alipokuwa Askofu mkuu wa Cantebury, alikuwa miongoni
mwa watu waliopinga mswada wa Lord Joffes wa kuwasaidia wagonjwa
wanaougua kupitia kisia kujitoa uhai ambao ulipingwa katika bunge la
mabwana mnamo mwaka 2006.
Anasema kuwa inawezekana kuwa mcha mungu na vilevile kuwasaidia wale wanaotaka kujitoa uhai.
lakini
katika taarifa yake hii leo katika gazeti la Daily Mail Lord Carey
alisema ''ukweli ni kwamba nimebadilisha uamuzi wangu''.
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapowekwa kwenye mtandao huu.LIKE HAPA