UNDANI JUU YA MTOTO ALIYEFICHWA UVUNGUNI MWA KITANDA
http://melckstudio.blogspot.com/2014/07/undani-juu-ya-mtoto-aliyefichwa.html
Msimamizi wa Nyumba hiyo akimuonyesha
Msimamizi huyo akitoka nje ya nyumba
hiyo na mwandishi wetu
Mwenyekiti wa kijiji hicho akihojiwa na mwandishi wetu
Dustans Shekidele mwandishio wa habari hii
Mtoto Devota akikunja sura kwa uchungu wa maumivu
Muuguzi akimfunga kidonda Devota
Na Dustans Shekidele,Morogoro.
SAKATA la
mtoto Devota Malole mwenye umri wa miaka 5 ambaye ni mlemavu
aliyeibuliwa baada ya kufichwa chini ya uvungu wa kitanda kwa muda wa
miezi mitatu huko Matongolo, Dumila,Tarafa ya Magole wilayani Kilosa
limeibua mambo mapya, baada ya kubaini kuwa aliyesababisha kuokolewa ni
mume wa mama wa binti huyo.
Mashuhuda
waliokuwepo wakati wa kufichuliwa kwa mtoto huyo, wakiwemo majirani na
wapangaji wa nyumba aliyokuwa akiishi, walisema mpangaji wa chumba
hicho, Masumbuko Mkwama (25), aliishi peke yake kwa muda mrefu kabla ya
miezi mitatu iliyopita, kuja na mwanamke aliyemzidi umri, Salah Mazengo
(36) aliyemtambulisha kama mke wake akiwa na watoto watatu.
Msimamizi
wa nyumba hiyo, Donata Sisie ambaye alidai mwenye nyumba anaishi
Morogoro mjini, alisema baada ya kumuhoji mwanamke huyo, alisema alikuwa
na watoto watano na kila mmoja alikuwa na baba yake na kwamba watatu
kati yao, walichukuliwa na wazazi wao na hivyo kubaki na wawili, Elias
mwenye umri wa miaka nane na mdogo wa mgongoni.
“Juzi
Julai 8, Masumbuko aliwafuata wapangaji wenzake watatu na kuwaeleza
kwamba mkewe ana mtoto mlemavu ambaye ni mgonjwa, lakini mwanamke huyo
hataki mwanaye atibiwe, jambo ambalo linamshangaza. Kwa pamoja, watu hao
walikwenda kutoa taarifa kwa Mwenyekiti wa Kitongoji, ambaye baada ya
kuelezwa juu ya mtoto huyo, aliamua kwenda polisi.
“Julai
10, mwaka huu, askari polisi pamoja na mwenyekiti huyo walikuja hapa
nyumbani na kumfichua mtoto huyo chini ya uvungu. Tokea siku ya tukio,
Masumbuko hajulikani alipo.
“Juzi
ulitokea mvutano mkali hapa kwani mama mzazi wa Sala alifika akitaka
kuchukuwa vyombo vilivyomo ndani ya chumba cha Masumbuko, mimi nilimzuia
kwa hoja kwamba ninachojua chumba ni cha mvulana hivyo nimevichukua
vitu vyake na kuvihifadhi kwangu hadi atakapofika.”
Mmoja
wa wapangaji wenzake na Masumbuko, Asha Mohamed alisema alipohamia yeye
na mumewe, walimkuta Masumbuko akiishi peke yake hadi miezi mitatu
iliyopita walipomuona akimleta mwanamke mtu mzima aliyekuwa na watoto
watatu, mmoja akiwa na ulemavu wa miguu.
Alisema alimuona mtoto mlemavu akiwa salama kwa siku moja tu, ile aliyofika na tangu hapo hakumuona tena.
“Alipokuja
alikaa naye hapa kwenye korido, sijamuona tena hadi juzi alipofichuliwa
akiwa tofauti na nilivyomuona mwanzo, kiukweli huyo mtoto alizaliwa
akiwa mlemavu na kwa mujibu wa maelezo ya mama yake, baba yake alimkana
baada ya kumuona na ulemavu.
“Niwe
mkweli kwenye hili, mtoto huyu alifichwa uvunguni tangu ahamie hapa,
hii inatokana pengine na ugumu wa maisha kwani kwenye chumba chao wana
kitanda futi nne na wanalala wanne baba, mama mtoto wao mkubwa Elias na
huyo mtoto wa mgongoni, kuna kipindi nilimuuliza Devota alikuwa wapi
aliniambia kuwa alimpeleka kwa bibi yake yaani mama yake anayeishi
kitongoji kinachofuata,” alisema Asha.
Kwa
upande wake, mwenyekiti wa kitongoji hicho, Dotto Hambosi alisema baada
ya kupewa taarifa na wananchi wake aliwasiliana na polisi, ambao kesho
yake walifika na kumkamata mwanamke huyo baada ya kukiri kuwa na mtoto
uvunguni mwa kitanda chake. Baadaye walimpeleka Kituo cha Polisi Dumila
kabla ya kumkimbiza katika Hospitali ya Wilaya ya Kilosa anakopatiwa
matibabu.
Juu
ya kazi za wazazi hao wawili, Hambosi alisema mwanaume anauza mishikaki
na mwanamke pombe za kienyeji katika kilabu cha pombe za kienyeji.
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapowekwa kwenye mtandao huu.LIKE HAPA