WAKIMBIZI SITA WAHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIEZI SITA AU FAINI YA SHILINGI ELFU THELATHINI KILA MMOJA
http://melckstudio.blogspot.com/2014/07/wakimbizi-sita-wahukumiwa-kifungo-cha.html

Baadhi
ya wakimbizi wa makazi ya Ulyankulu wakitoka kwenye Chumba cha Mahakama
ya hakimu mkazi baada ya kusomewa hukumu ya kifungo cha miezi sita jela
au kulipa faini ya shilingi ya elfu thelathini kila mmoja
Na mwandishi wetu Tabora.
Watu
sita ambao ni wakimbizi katika makazi ya Ulyankulu wamehukumiwa
kutumikia adhabu ya kifungo cha miezi sita au kulipa faini ya shilingi
elfu thelathini kila mmoja baada ya kupatikana na makosa ya kutoroka
eneo la makazi ya wakimbizi Ulyankulu pamoja na kukutwa wakifanya
shughuli za kiuchumi kinyume na kifungu cha makosa ya uhamiaji nchini.
Watu hao
sita ambao walifikishwa kwa mara nyingine katika makahama ya hakimu
mkazi mkoa wa Tabora ambapo wakili wa upande wa mashtaka Bw.Salehe Mgeni
aliieleza mahakama kuwa mnamo tarehe 25 machi mwaka huu wakimbizi hao
walikamatwa wakiwa wanafanya kazi ndani ya hifadhi ya msitu wa Ugalla
katika Tarafa ya Ussoke wilaya ya Urambo, kosa ambalo liliunganishwa na
lile na kutoka nje ya eneo la makazi ya Ulyankulu bila kibali cha Mkuu
wa makazi.
Pamoja na
kosa hilo la kwanza la kujihusisha na shughuli za kiuchumi kiunyume cha
sheria ya Uhamiaji nchini washitakiwa hao sita walikiri makosa hayo
mbele ya hakimu mkazi mkoa wa Tabora Bw.Jackton Rushwela na hivyo
kuhukumiwa adhabu ya kifungo cha miezi sita au kulipa faini ya shilingi
elfu thelathini kila mmoja.
Aidha
wakimbizi hao waliohukumiwa ni Mapili John,Jeremia Matoli,Kitenge
Sayumba,Obed Ndabasigiye,Enock Sayumo na Zarubali Sanzugwimo ambao
walikamatwa katika msitu huo wa hifadhi Ulyankulu walikuwa wakifanya
shughuli za uchanaji wa mbao.
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu.BOFYA HAPA