WASHUHUDIE LIVE MAJANI, PROFESSOR J NA DIAMOND WAINGIA STUDIO UPYA KUIONEGESHA ‘KIPI SIJASIKIA’ KWAAJILI YA VIDEO
http://melckstudio.blogspot.com/2014/07/washuhudie-live-majani-professor-j-na.html
Itakapotoka
video ya wimbo wa Professor J ‘Kipi Sijasikia’ aliomshirikisha Diamond
Platnumz, unaweza ukasikia sauti mpya ambazo hukuzisikia awali kwenye
wimbo huo uliotoka miezi kadhaa iliyopita.


Picha za set ya video hiyo
Akiongea
na East Africa Radio hivi karibuni, Professor alisema Diamond
alijisikia kufanya marekebisho kwenye wimbo huo hivyo watu wategemee
vitu vizuri zaidi kwenye video. “Audio tunakubali imeshatoka na
imekubalika lakini video bado ina nafasi ya kuweza kuwekewa chochote
kinachoweza kuboreshwa zaidi. Kwahiyo tunaweza kuboresha zaidi kwenye
video kupitia audio kwasababu producer tunaye na anatuonesha ushirikiano
kwa asilimia kubwa.”

Professor na Diamond wakiwa location kushoot video hiyo
Video hiyo imeongozwa na Adam Juma.
Source:BONGO5.COM
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapowekwa kwenye mtandao huu. LIKE HAPA