WIMBI LA MADAWA YA KULEVYA, MNAGERIA ADAKWA NAIROBI BAADA YA RUBANI KUUGUA
http://melckstudio.blogspot.com/2014/07/wimbi-la-madawa-ya-kulevya-mnageria.html
Mwanamume
mmoja Raia wa Nigeria imebidi alazwe kwenye hospitali ya taifa ya
Kenyatta Nairobi Kenya baada ya kugundulika alikua na mzigo wa dawa za
kulevya wa vidonge 57 tumboni mwake.Huyu jamaa alikua anazisafirisha
hizi dawa kutoka Lagos kwenda Bangkok lakini ghafla akaanza kupata
maumivu baada ya kuchelewa kufikisha mzigo aloubeba tumboni mwake baada
ya ndege waliyokua wakisafiria kutua Nairobi kwa dharura.
Ilitua kwa
dharura baada ya rubani kuumwa ghafla hivyo kulazimu ndege kutua Nairobi
kisha abiria wote kupelekwa hotelini na hapo ndio Mnigeria huyu akaanza
kuhisi maumivu makali tumboni.
Simon Ithae ambae ni mkuu wa mawasiliano hospitali ya Kenyatta amesema ‘alitueleza amemeza vidonge na alikua akiamini ndicho chanzo cha maumivu hivyo alipoona hawezi kustahamili aliita Polisi akidai ameumizwa na anahitaji kupelekwa hospitali lakini lengo lake ni apange njama na madaktari kutoa dawa za kulevya bila yeye kukamatwa na aendelee nazo na safari lakini mipango yake haikufanikiwa kwa sababu Madaktari walimpa chakula ili kutoa dawa hizo na kisha wakawapa taarifa Polisi.
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapowekwa kwenye mtandao huu.LIKE HAPA