BIFU KATI CLOUDS FM NA UKAWA:TUNDU LISSU AIBUKA AWAVAA NA ASEMA MAZITO,SOMA HAPA KUJUA ALICHOKISEMA
http://melckstudio.blogspot.com/2014/08/bifu-kati-clouds-fm-na-ukawatundu-lissu.html
Pichani ni Mkurugenzi wa Clauds Media Group Joseph Kusaga picha na maktaba
Na Karoli Vinsent
SAA
chache kupita Baada Radio ya Clauds Fm kutangaza
Rasmi kutozisoma Habari zozote zinazowahusu Wajumbe wanaunda umoja wa
Kutetea Katiba ya Wananchi UKAWA, kwa kile wananachodai Umoja huo hauna
jipya bali unataka umaharufu tu.
Kauli
hiyo ya ambayo inakwenda kinyume na Maadili ya Vyombo vya Habari
imetolewa leo na Mtangazaji wa Kipindi cha Power breakfast Babla hassani
wakati wakichambua magazeti ya siku ambapo alisema kwa
sasa hawatazisomi habari zozote zinazohusu umoja huo wa Ukawa kwa madai
umoja huo ni wabinafsi na hawana jipya bali wanataka Umaharufu.
Naye
Mwanasheria wa Umoja wa kutetea katiba ya Wananchi UKAWA ,Tundu Lissu
amewavaa na kusema Radio hiyo inajimaliza na ndio itakuwa inaonekana
wazi inapendelea Upande moja Kisiasa.
Kauli
hiyo Tundu Lissu,ameitoa mda huu wakati alipokuwa anaongea na
Mwandishi wa Mtandao huu,Kuhusu wao Ukawa wamepokeaje Taarifa hiyo ya
kutosomwa Habari zao kwenye Radio hiyo.Ambapo Lissu alisema hizo
taarifa anazisikia na kama ni kweli wametangaza hivyo watakuwa
wamejimaliza.
“Kwanza
nimezisikia hizo taarifa na kama kweli aliyosema huyo mtangazaji ndio
msimamo wa Radio nzima basi watakuwa watu wa Ajabu sana maana leo Nchi
nzima habari ya Mjini ni Ukawa,leo utasemaje ukawa ni wabinafsi wakati
wasomi na watu wengine wanaungana na sisi leo inakuwaje Radio hiyo
iseme hivyo kama wako upande mmoja wa Kisiasa weseme”alisema Lissu.
Tundu
Lissu,ambaye naye ni Mjumbe wa Bunge maalum la Katiba alizidi kusema
yeye sio mwanahabari bali anachokijua huo utakuwa msimamo wa Radio nzima
na wao Ukawa hawata ogopa na kuacha kuwatetea wananchi kwani wako kwa
ajili ya kuwakomboa wananchi na hawezi kukatishwa na tamaa na watu
wachache wenye maslai ya upande mmoja.
“Harafu
inashangaza sana leo nchi nzima inazungumzia Ukawa harafu mtua aseme
leo Ukawa utotangaza habari zao kwa misingi hipi?”alihoji Tundu lissu.
Kauli
hiyo ya Tundu Lissu,imetolewa saa chache kupita baada Mtangazaji wa
kipindi cha Power Breakfast Babla Hassani,kutangaza Rasmi kwamba
hawatasoma Habari zozote zinazohusu Umoja huo.
“Mimi
Naona kusoma Story zinahusu Ukawa tunawapa kiki tu wao siwamekuwa
kutupotezea kutorejea Bunge I whon doing,vile vikao vinawanufaisha
watanzania wote wao ni wabinafsi tu,the best ican do tuwapotezea Habari
zao, na ukiona habari inahusu Ukawa tu usisome hapa kwenye Redio,na
wakae huko nje atuwataki Ukawa bungeni”alisema Babla Hassani.
Kauli
hiyo ya iliungwa Mkono pia na Mtangazaji wa mwengine wa kipindi
hicho, Paul Jems anayejulikana kwa jina la Umaharufu “PJ” naye alisema
kwanzia sasa hatazisoma habari zozote zinazohusu Umoja huo kwani
wanapoteza pesa za wananchi bure kwa kususia bunge hilo.
Msimamo
huo wa Watangazaji hao unakwenda Kinyume na Mmiliki wa Radio hiyo ya
Clauds Fm Joseph Kusaga alipokuwa anahojiwa na kipindi kimoja cha
runinga kutoka nchini Uingereza kinachojulikana,The Sporah Show ambapo
katika kipindi hiko alisema Radio yake haina upande wowote wa
Kisiasa na kuongeza ni Redio huru inayofanya kazi bila kushabikia upande
wowote.