DAKTARI FEKI AMEKAMATWA MANYARA AKIDAI NI DAKTARI WA MAGONJWA YA MOYO
http://melckstudio.blogspot.com/2014/08/daktari-feki-amekamatwa-manyara-akidai.html
opo la madaktari katika
hospitali ya rufaa ya mkoani Manyara kwa kushirikiana na polisi wamefanikiwa
kumnasa mkazi wa jijini Dar-es-salaam Bw Godlove Sozigwa akituhumiwa kuomba
kufanya mazoezi ya kutibu kwa muda kama daktari wa magonjwa ya moyo na figo kwa
kutumia vyeti bandia wakati akitambua kuwa yeye si mtaalam wa tiba.Bw Godlove Sozigwa kabla
ya kukamatwa kwake asubuhi kufuatia jopo hilo la madaktari kubaini kuwa vyeti
alivyoviwasilisha katika hospitali hivyo julai 31 ni bandia na hata hivyo
alipoitwa na kufanyiwa mahojiano amedai huku akionyesha ukomavu wa kujieleza
taaluma hiyo aliipatia katika chuo cha sayansi, tiba na utafiti cha Muhimbili
na kufuzu hata hivyo alibahatika serikali kumpeleka nchini India kwa mafunzo
zaidi kusomea dawa zaidi.Kwa upande wake mganga mfawidhi wa hospitali ya rufaa mkoani Manyara Dr Peter Mshali akizungumza na EATV baada ya kukabidhiwa kwa polisi ili kufanyiwa upelelezi amesema katika mahojiano na jopo la madaktari walibaini vyeti hivyo ni bandia aidha pia mtuhumiwa Dr huyo Godlove Sozigwa si mtaalam kulingana na maelezo yake bali ni tapeli na hatari endapo angebahatika kupata nafasi hiyo.
Naye kamanda wa polisi
mkoani hapa ACP Deusdedit Nsimeki amekiri na katika mahojiano amesema polisi
imebaini baada ya kumfanyia mahojiano na upekuzi kumkuta na kompyuta
mpakato(laptop) muhuri wa kuchonga wa hospitali ya rufaa ya Muhimbili, koti na
vyeti mbalimbali, lakini wanafanya upelelezi zaidi kabla ya kumfikisha
mahakamani.
