Ebola:Liberia yatangaza hali ya dharura
http://melckstudio.blogspot.com/2014/08/ebolaliberia-yatangaza-hali-ya-dharura.html

Rais wa Liberia ametoa wito wa hatua zaidi kuchukuliwa kuzuia maambukizi
Liberia imetangaza hatua za dharula dhidi ya ugonjwa wa Ebola kufuatia kasi kubwa ya kuenea kwa ugonjwa huo.
Rais wa Liberia Hellen Sirleaf amesema nchi yake
kwa sasa inakabiliwa na tatizo la ugonjwa huo huku baadhi ya wananchi
wakiwa na uelewa mdogo kuhusiana na hatua za kujikinga na ugonjwa huo.
Rais Sirleaf Johnson amelaumu ukosefu wa elimu na umaskini kama chanzo kikubwa cha maabukizi ya Ebola
Hatua hiyo ya Liberia inakuja huku wataalamu wa afya toka shirika la afya Ulimwenguni WHO wakikutana Geneva, Switzerland, kujadili mbinu za kukabiliana na ugonjwa huo.
Katika mkutano huo wa siku mbili wataalamu hao watajadili wautangaze ugonjwa wa Ebola kuwa janga la kidunia.

Wauguzi wamekuwa wakiwaelimisha wananchi kuhusu namna ya kujikinga na maambukizi
Marekani na mataifa ya ulaya imesema kuwa inatafuta mbinu za pamoja katika kutokomeza ugonjwa huo.
Ugonjwa wa Ebola kwa nchi umebainika kuwepo Guinea, Sierra Leone na Nigeria ambapo zaidi ya watu 930 wamekufa kutokana na ugonjwa huo.

Umma umekuwa ukihamasishwa kuhusu ugonjwa huo hatari
Chanzo bbc
kama
huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe
zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu.LIKE HAPA