MSANII LINEX:NITAGOMBEA UBUNGE KASULU MJINI MWAKANI,ZITO NDO MWENYEKITI WA CHAMA CHANGU CHA ACT

Msanii Linex :Zitto Kabwe ndo mwenyekiti wa ACT

Katika hali ya kushangaza na ya kustua wengi,msanii maarufu wa mziki wa bongofravour kutokea mkoani Kigoma Linex,ametangaza nia ya kuwania ubunge mwakani katika jimbo la kasulu mjini,jimbo ambalo kwa sasa linaongoewa na mbungz Moses Machali wa NCCR MAGEUZI.

Msanii huyo anaetamba kwa nyimbo mbalimbali za kizazi kipya ameyasema hayo mchana huu kupitia Radio Clouds Fm katika kipindi cha XXL segment imayotamgazwa na mtangazaji Sud Brown maarufu kama Makorokocho,
m
Linex alikwenda mbali kwa kumtangaza mbunge wa Kigoma kaskazini Zitto kabwe kama mwenyekiti wa chama kipya cha ACT,Linex alisema"mimi ni mheshimiwa mbunge mtarajiwa wa jimbo la Kasulu"mtangazaji alipomuuliza atagombea ubunge kupitia chama gani alisema kupitia ACT huku akisema mwznyekiti wa ACT ni Zitto Kabwe,ambaye wameamua kumuunga mkono kupitia ACT kufuatia na yeye kuwaunga mkono kupitia wimbo wa Lekadutigite.

Kauli ya msanii huyo ni kama imekuja kukamilisha uvumi wa sikunyingi kwamba Zitto kabwe ni mmoja ya waanzilishi wa chama hicho na kwamba anatarajia kuhimia rasmi chama hicho ambacho wengi ya wanachama wake ni wale waliofukuzwa CHADEMA kwa tuhuma mbalimbali zikiwemo tuhuma za usaliti,katika taaeifa hizo za awali zilizomuhusisha Zitto na ACT zilidai atajiunga rasmi na ACT mwezi wa 9/2014 wakati wa uzinduzi wa chama hicho,uzinduzi unaotarajiwa kufanyikia jijini Mwanza na mgeni rasmi kwa mujibu wa taarifa hizo anatajwa atakuwa ni Julius Malema kutoka Afrika kusini ambaye naye alifukuzwa kutoka katika chama chake cha zamani cha ANC ambapo alikuwa ni mwenyekiti wa vijana chama hicho tawala nchini Afrika kusini.


 
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu.LIKE HAPA

Related

SIASA 7766280006668902025

Asia - Leo

MZIWANDA - MSONDO NGOMA

TONBOY

TONBOY

CONTACT

Melck Studio
Tel : +25578920034
+255757605268
E-mail : melckstudio@gmail.com

SHOW LOVE TO THIS

Hot in week

Recent

Comments

Visitors


web stats
item