MTOTO MWENYE UMRI WA MIAKA SITA AMEFARIKI BAADA YA KUKANYAGWA NA GARI LA MAMAKE
http://melckstudio.blogspot.com/2014/08/mtoto-mwenye-umri-wa-miaka-sita.html

Bulutito Shodipe alikuwa na umri wa miaka sita
Bolutito
Shodipe mwenye umri wa miaka sita aligongwa na mamake aliyekuwa
anajaribu kuegesha gari lake nje ya kituo cha treni cha Hounslow West
Tube nyakati za asubuhi Jumatano wiki hii.
Juhudi za kuokoa maisha ya Bolitito katika eneo hilo ziliambulia patupu kwani alisemekana kuaga dunia alipofikishwa hospitalini.
Taarifa kutoka kwa familia ya Bolitito ilisema kuwa wanajaribu kuikubali hali iiliyowakuta kutokana na ajali hiyo mbaya.
Familia
hiyo inayoishi eneo la Hayes Magharibi mwa London, iliongeza kusema:
"Bolutito alikuwa mtoto wetu wa kwanza na alikuwa nuru kwetu. ''
"alikuwa mrembo, mwenye maadili mema, na mpenzi wa Ballet, na tutamkosa sana.''
Polisi
walithibitisha kwamba kifo cha mtoto huyo kilikuwa ajali kwani walifika
wote katika kituo cha treni na mamake, ila mtoto aligongwa na kufariki
wakati mama akijaribu kuegesha gari lake.
Polisi wanachunguza tukio hilo
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu. LIKE HAPA