MWANDISHI WA HABARI RAIA WA MAREKANI AUAWA SYRIA
http://melckstudio.blogspot.com/2014/08/mwandishi-wa-habari-raia-wa-marekani.html
![](http://a.files.bbci.co.uk/worldservice/live/assets/images/2014/08/19/140819231627_james_foley_512x288_afp.jpg)
James Foley enzi za uhai wake akiwa na vitendea kazi vyake.
Kikosi
cha kiislam cha kijeshi chenye msimamo mkali kimeachilia video
inayoonesha mauaji ya mwandishi habari mwenye asili ya Marekani. James
Foley alipotea tangu alipokamatwa mateka na kushikiliwa nchini Syria
miaka miwili iliyopita na sasa ameuawa.
Ikulu
ya Marekani imesema inaifanyia uchunguzi wa kina video hiyo na
ikithibitika kwamba mwandishi huyo wa habari ni wa taifa hilo ,serikali
ya Marekani itataka ufafanuzi wa kina ilikuaje na kwanini James Foley
auawe.
Katika
mtandao wa kijamii wa Facebook familia ya mwandishi huyo iliandika
kuwa’tunajua kwamba wengi wenu mnasubiri uthibitisho ama majibu ya
maswali yenu,tafadhalini muwe watulivu mpaka nasi sote tupate taarifa
tunazo tamia,na tunaomba muendelee kumbumbuka Foleys na kumwombea kila
siku.’’
Katika
video hiyo iliyobeba ujumbe unaosomeka kua ujumbe kwa
Marekani,mwandishi huyo pia alionekana akiwa chini ya ulinzi wa mtu
aliyekua amevalia kinyago usoni,askari huyo alikua aku akizungumza ndani
ya lafidhi yenye athari za Uingereza,akisema kua kifo cha mwandishi
huyo ni matokeo ya mashambulizi ya magurunedi yalowalenga wa Iraq.
>>>>>BBC
>>>>>BBC
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu. LIKE HAPA