NI VILIO NA HUZUNI WAKATI MIILI YA WATU WALIOKUFA KWENYE NDEGE YA MALAYSIA IKIPOKELEWA
http://melckstudio.blogspot.com/2014/08/ni-vilio-na-huzuni-wakati-miili-ya-watu.html

Miili 20 ya wahanga wa ndege ya Malaysia MH17 imewasili Kuala Lumpur
Malaysia
iko katika siku ya maombolezi ya kitaifa baada ya kupokea miili 20 ya
wahanga wa mkasa wa ndege ya Malaysia MH17 iliyotunguliwa Ukraine mwezi
uliopita.
Miili ilipokelewa na kupewa heshima za kitaifa.
Majeneza
yalikuwa yamefunikwa na bendera za taifa na ilibebwa na wanajeshi kabla
ya kusafirishwa kwa magari ya kubeba maiti iliyozipitishwa karibu na
mfalme na waziri mkuu kabla ya kukabidhiwa kwa familia husika.
MH17 iliangushwa katika eneo la waasi Mashariki ya Ukraine mwezi uliopita.
Machi
mwaka huu ndege nyingine ya Malaysia ilitoweka katika bahari hindi
amesema kuwa shirika hilo la ndege linaendelea kutatizwa na matukio hayo
mawili.

Maombolezi Kuala Lumpur
Wasafiri wote 298 waliokuwa katika ndege hiyo ya MH17 walifariki 43 kati yao wakiwa raiya wa Malaysia.
Ndege iliyobeba miili hiyo ilikuwa imetengwa kwaajili ya shughuli hiyo kutoka Amsterdam na kutua saa nne saa za huko.
Bendera ya taifa itapepea nusu mlingoti kote nchini na dakika moja ya kimya itazingatiwa.
Kikundi
kidogo cha wanajeshi wa Malaysia kilienda hadi karibu na ndege hiyo
kulinda majeneza hayo yalipokuwa yakitolewa kwa ndege huku magari
makubwa meupe ya mazishi yakiwa yamepangwa kuzipokea miili hiyo.
Majeneza yote yamefunikwa kwa bendera ya taifa na miili mitatu ya hiyo 20 imechomwa nchini Uholanzi.

Baadhi ya Miili 20 ya wahanga wa ndege ya Malaysia
MH17 imezikwa Kuala Lumpur
New
Straits Times ilisema sekta ya uchukuzi ya umma nchini humo ikiwemo ile
ya reli ya taifa na reli moja ya Kuala lumpur zitasimamisha shughuli
zao kuzingatia dakika mbili za kimya kwa heshima ya wahanga wa mkasa
huo.
Vibanda
maalum kwenye barabara kuu vitakuwa na ishara za kielektroniki
kuwaeleza madereva washuke kutoka kwa magari yao ilikutoa heshima.
Msemaji
wa ndege za Malaysia alisema kwamba kampuni hiyo ingepanga kipindi cha
maombi ambacho kingefanywa wazi kwa mtu yeyote ili kutoa maombi na
heshima zao kwa walioaga.
Akiongeza alisema kwamba kampuni hiyo ya ndege za Malaysia imehuzunishwa sana na tukio hilo la kuogofya .
Aidha imekuwa muda mrefu wa kungoja kwa familia na marafiki wa wasafiri na wafanyakazi waliokuwa katika ndege MH17.

Baadhi ya Miili 20 ya wahanga wa ndege ya
Malaysia
MH17 imezikwa Kuala Lumpur
Hii ni mara ya kwanza Malaysia inaendeleza siku ya maombolezi ya taifa kwa wananchi wa kawaida.
Heshima hiyo kitamaduni imekuwa ikipewa familia ya mfalme na wakuu serikalini.
Kufikia
sasa waathiriwa 28 wa Malaysia wametambuliwa nchini Uholanzi ambako
utafiti wa kimataifa kuhusiana na kuanguka kwa ndege hiyo mashariki mwa
Ukraine unaendelezwa.
Zaidi
ya majeneza 200 iliyo na mabaki ya waathiriwa kufikia sasa yamepelekwa
Uholanzi lakini uchunguzi unazuiliwa na mapigano yanayoendelea kati ya
majeshi ya serikali ya Ukraine na waasi yanayoiunga mkono Urusi karibu
na eneo ambalo ndege hiyo ilianguka.
CHANZO BBS SWAHILI
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu. LIKE HAPA