Obama atetea Marekani kushambulia ISIS
http://melckstudio.blogspot.com/2014/08/obama-atetea-marekani-kushambulia-isis.html

Rais Obama amesema hataruhusu wapiganaji wa siasa
kali wa madhehebu ya Sunni kuunda himaya yao nchini Syria na Iraq; na
ndege za Marekani zitafanya mashambulio zaidi ikihitajika.
Rais Obama aliliambia gazeti la New York Times,
ni masilahi ya Marekani kuwazuwia wapiganaji wa ISIS wasisonge mbele na
piya ina wajibu kuzuwia mauaji ya kimbari.Katika hotuba yake ya kila juma, alisema wapiganaji hao wanawateka wanawake na kuwafanya watumwa wao na wanatishia kuiangamiza jamii ya madhehebu ya Yazidi yenye waumini wachache.
Alisema mashambulio ya ndege yanaweza kumaliza kuzingirwa kwa wakimbizi wa Yazidi waliokimbilia milimani.
Ndege za Marekani kwa mara ya pili zimedondosha msaada wa dharura kwa maelfu ya wakimbizi wa madhehebu ya Yazidi ambao wamenasa mlimani, kaskazini mwa Iraq.
Walikimbia makwao wakati wapiganaji wa ISIS walipokaribia.
Chanzo bbc
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu.LIKE HAPA