PASTOR MYAMBA APATA AJALI MBAYA YA GARI
http://melckstudio.blogspot.com/2014/08/pastor-myamba-apata-ajali-mbaya-ya-gari.html
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjI0fAQpxDo-vixdTqLQBdFcwymZdHnkh2vhFpgM_V37b9icc9SxucNFYSkQJ6Y1oKNE_p0-iPc8O_Xk9KnjUFmdLlWxXG1ATR8eex4Nd36O1PBP-gsc9gcHCOOJs67t9FLJSe7dMde-g9s/s1600/1MYAMBACAR.jpg)
Taswira baada ya ajali hiyo.
STAA
wa filamu za Kibongo, anayepatia zaidi kuigiza kama Mchungaji, Emmanuel
Myamba ‘Pastor Myamba’ amepata ajali baada ya gari lake aina ya Toyota
Creasta kugongwa na gari lingine leo mchana katikati ya Boko na Bunju
jijini Dar es Salaam.
Katika ajali hiyo, hakuna mtu aliyejeruhiwa zaidi ya magari hayo mawili kuharibika.
Kwa
mujibu wa Pastor Myamba, dereva aliyekuwa akiendesha gari lililogonga
gari lake alitokomea na kuacha gari lake eneo la tukio baada ya kugundua
kuwa ndiye aliyekuwa na makosa.
Magari yote mawili yamevutwa na 'breakdown' kisha kupelekwa kituo cha polisi Tegeta.
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu. LIKE HAPA