Tabiti zapigwa marufuku Old Trafford
http://melckstudio.blogspot.com/2014/08/tabiti-zapigwa-marufuku-old-trafford.html

Uwanja wa Manchester United Old Trafford
Klabu ya soka ya Manchester
United imepiga marufuku uingizwaji wa tabiti au (Tablets) na komputa za
Laptop kwa watakaokuwa wanaingia katika uwanja wake.
Klabu hiyo inasema imechukua hatua
hiyo,kuambatana na taarifa za kijasusi ikiongeza kwamba kikwazo hicho
kinaambatana pia na mikakakti mipya ya ukaguzi wa vifaa vya elektroini
katika viwanja vya ndege.Ilisema kuwa kinyume na hali ilivyo katika viwanja vya ndege, haitawezekana kuhakikisha ikiwa vifaa vinavyoletwa na mashabiki ikiwa ni ghushi kwa kutaka waviwashe.

Mashabiki wa United
Taarifa kwenye mtandao wa klabu hiyo, imesema marufuku hiyo itahusisha tabiti kubwa na ndogo, pamoja na vifaa vingine vikubwa vya elektroniki.
Lakini Smartphones zinaruhusiwa ila kwa masharti fulani.

Maafisa wa ligi ya Premier wanasema hawajahusika na marufuku hiyo
Aliongeza kwamba wasiwasi kuwa klabu hiyo haitaki mashabiki kurekodi video za mechi zinapokuwa zinaendelea na kuwazuia mashabiki wengine kutizama mechi, hauna msingi.
Msemamji wa ligi ya uingereza naye amesema kwamba wao hawajahusika kivyovyote na marufuku hiyo.
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu. LIKE HAPA