TAZAMA PICHA: VIBAKA WACHOMWA MOTO HADI KUFA DAR!
http://melckstudio.blogspot.com/2014/08/tazama-picha-vibaka-wachomwa-moto-hadi.html
Baadhi ya wananchi wakishuhudia jinsi miili hiyo inavyoteketea.
Vijana wawili wakazi wa Jiji la Dar es Salaam ambao hawakufahamika majina
yao, wanaodaiwa kuwa ni vibaka alfajiri ya leo wameuawa kwa kuchomwa
moto na wananchi wenye hasira kali baada ya kumpora pochi dada mmoja
mkazi wa Tabata Liwiti. Shuhuda wa tukio hilo ambaye hakupenda kutaja jina lake alisema baada ya vibaka hao kumpora pochi dada huyo, walitaka
kutoweka na bodaboda ndipo wananchi walifanikiwa kumkamata aliyeipora
pochi hiyo akaanguka chini wakaanza kumpa kipigo huku mwenzake
akifanikiwa kuondoka.
Matairi yaliyotumika kuwachomea vibaka hao yakiungua.
Miili hiyo ikiteketea kwa moto

Kama waswahili wasemavyo za mwizi arobaini, kibaka huyo aliyekuwa akiendesha bodaboda kwa kasi, hakufika mbali pikipiki yake ikapata pancha naye akakamatwa na kuanza kupewa kichapo kisha walikusanywa pamoja wakavishwa matairi na kuchomwa moto.
Baada ya kuteketea kwa moto, polisi walifika eneo la tukio wakachukua mabaki ya miili ya vibaka hao na kuipeleka tatika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
PICHA NA GPL
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu. like hapa