WANAJESHI 480 WA NIGERIA WAKIMBILIA CAMEROON BAADA YA KUZIDIWA NGUVU NA BOKO HARAM
http://melckstudio.blogspot.com/2014/08/wanajeshi-480-wa-nigeria-wakimbilia.html
![](http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2014/07/30/140730160117_nigeria_512x288_reuters_nocredit.jpg)
Majeshi 480 wa Nigeria watorokea Cameroon
Wanajeshi
480 wa Nigeria wametorokea maisha yao nchi jirani ya Cameroon kufuatia
makabiliano makali dhidi ya wapiganaji wa kundi la kiislamu la Boko
Haram.
Msemaji
wa jeshi la Cameroon Luteini Kanali Didier Badjek amethibitisha kisa
hicho na kusema kuwa wamepokonywa silaha na sasa wamewekwa katika shule .
Mapigano
hayo yanawadia saa chache tu baada ya wapiganaji hao wa Boko Haram
kutoa kanda ya video ambayo walitangaza kuundwa kwa himaya ya Kiislamu
kaskazini Mashariki mwa Nigeria.Mapigano hayo yanaendelea karibu na mji
ulioko mpakani wa Gamboru Ngala.
![](http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/09/07/130907044759_nigeria_army_soldiers_512x288_ap_nocredit.jpg)
Wanajeshi hao walikuwa wakikabiliana na wapiganaji wa
Boko Haram
Kiongozi
wa Boko Haram Abubakar Shekau alizungumza kwenye kanda ya video
iliyotolewa ili kupongeza wapiganaji wake kwa kuchukua udhibiti wa mji
wa Gwoza mapema mwezi huu.
Haijabainishwa
iwapo Bwana Shekau ameahidi kutii Muungano wa wapiganaji wa kundi la
kiislamu la Islamic State inayotawala sehemu kubwa ya Kaskazini mwa Iraq
na Syria.
Msemaji
wa Jeshi la Nigeria Chris Olukolade alipinga tangazo hilo akisema kuwa
''hakuna hata nchi moja ya taifa hilo iliyotwaliwa na kuwa Nigeria ni
moja. ''
![](http://a.files.bbci.co.uk/worldservice/live/assets/images/2014/08/21/140821200246_boko_haram_512x288_n_nocredit.jpg)
Kiongozi wa Boko Haram Shekao ametangaza himya ya
KIislamu Kaskazini mashariki mwa Nigeria
Maelfu ya watu wameuwawa kaskazini mashariki mwa Nigeria tangu 2009, wakati Boko Haram ilipoanza uasi wake.
Gwoza, iliyokuwa na wakazi 265,000 katika sensa iliyopita, ndiyo mji mkubwa zaidi ulio chini ya utawala wa Boko Haram.
Imepeperusha bendera zake juu ya Kasri ya Emir wa Gwoza, kiongozi wa kiasili wa mji huo, wakazi wanasema.
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu.LIKE HAPA