http://melckstudio.blogspot.com/2014/08/wema-sepetu-akerwa-na-kauli-ya-diamond.html
KAULI ya
nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kwamba hawezi
kuoa kamwe, inadaiwa kumchefua mwandani wake, Wema Isaac Sepetu
‘Beautiful Onyinye’
Kwa
mujibu wa mtu wa karibu wa mastaa hao, Wema hakufurahishwa na habari
hiyo kwa sababu anajua yeye ndiye mke mtarajiwa wa Diamond.
Ilidaiwa
kwamba, Wema alijikuta akipoteza ile furaha ya kwamba wawili hao
wangefunga ndoa mwezi huu (Agosti) kama ilivyotabiriwa na mnajimu
maarufu Bongo, Maalim Hassan Yahya Hussein.
Baada ya kauli hiyo ya Diamond na kutotimia kwa utabiri wa Maalim Hassan
kwa
sababu hakuna hata dalili za maandalizi ya tukio hilo muhimu kwenye
maisha ya mwanadamu, Wema ameanza kukata tamaa, lakini amesema hawezi
kulazimisha ndoa kwa mwanaume kwa kuwa si utamaduni wa wanawake wa
Kitanzania wala Kiafrika.
Unajua
Kibongobongo au hata Kiafrika hai-sound vizuri na pengine haiwezekani
kwa mwanamke kulazimisha kuolewa kama mwanaume hataki. Hicho ndicho
kilichomtibua Madam (Wema) baada ya kusoma alichokisema Diamond
kilisema chanzo hicho na kuongeza:
Wema
amehisi yeye ni girl lover (mpenzi) tu kwa Diamond na si wife material
(mke mwema) kwa hiyo anawaza sana kuhusiana na ishu hiyo japo mahaba
niue kati yao yanaendelea, lakini anafikiria kuchukua uamuzi mzito.
Baada
ya kuinyaka ishu hiyo, gazeti hili lilimtafuta mlimbwende huyo
anayeshikilia Krauni ya Miss Tanzania 2006 ili kumsikia mwenyewe ambapo
alifunguka yake ya moyoni.
Mwanadada huyo alisema kuwa kwa sasa haumizi tena kichwa kuhusu suala la ndoa na Diamond na kwamba hana haraka nalo.
Mimi naamini sana mambo ya utabiri, lakini siumizi kichwa na suala la kuolewa na Diamond na kamwe siwezi kumlazimisha anioe.
Kikubwa
katika mapenzi ni upendo wa kweli ambao ananionesha bila kipimo. Wala
sina papara, hata kama mtabiri kasema ndoa yetu ni lazima ifungwe mwaka
unaogawanyika kwa mbili kwa maana ya mwaka 2016 kama itashindikana mwezi
huu, hilo kwangu si tatizo la kunifanya nililie kuolewa na Chibu
(Diamond).
Ninachojua
mimi Mungu ndiye anapanga yote na kama ndoa ipo ipo tu maana kuna watu
wapo kwenye ndoa na hawana upendo wa kweli kama tulionano sisi
alisema Wema.
Kikubwa
katika mapenzi ni upendo wa kweli ambao ananionesha bila kipimo. Wala
sina papara, hata kama mtabiri kasema ndoa yetu ni lazima ifungwe mwaka
unaogawanyika kwa mbili kwa maana ya mwaka 2016 kama itashindikana mwezi
huu, hilo kwangu si tatizo la kunifanya nililie kuolewa na Chibu
(Diamond).
Ninachojua
mimi Mungu ndiye anapanga yote na kama ndoa ipo ipo tu maana kuna watu
wapo kwenye ndoa na hawana upendo wa kweli kama tulionano sisi
alisema Wema.
Paparazi
wetu alimtwangia simu mama yake Wema, Mariam Sepetu na kumuuliza mambo
mawili, kuhusu bintiye kuvishwa pete ya ndoa na Diamond na suala la
Mbongo Fleva huyo kusema hataoa kamwe!
Mimi
niseme nini? Sina la kusema kuhusu Wema. Mambo yake ni yake mwenyewe na
huyo Diamond wake. Kwanza kwa nini mnipigie mimi, si mumtafute yeye
mwenyewe?
alisema mama huyo kwa sauti ya utulivu.
Katika
hali ya kushangaza, mama Diamond, Sanura Kasim ‘Sandra’ ameonekana
kunawa mikono kwa kauli aliyowahi kuitoa siku za nyuma kuhusu mtoto wake
na masuala ya kutooa au kuoa.
Nasibu
ni mtu mzima sasa, siwezi kumpangia lolote kuhusu kuoa au kutooa.
Wakati ukifika, anaweza kusema lolote ambalo ataliona ni zuri katika
maisha yake.
Kuhusu Diamond kumvisha pete ya ndoa Wema, tendo ambalo lilifanyika hivi karibuni wakiwa nchini Afrika Kusini,
shehe mmoja ambaye aliomba hifadhi ya jina lake ambapo alisema alichokifanya Diamond kwa Wema ni usanii.
Diamond
amemfanyia usanii mwenzake. Pete gani bila kufunga ndoa. Halafu katika
Uislam, hakuna tendo la wanandoa kuvalishana pete, hayo mambo
wanayafanya wenyewe
alisema shehe huyo.
Wema
alipopewa nafasi ya kuizungumzia pete hiyo alisema Diamond aliipenda tu
akaamua kumnunulia na kumvisha lakini haihusiani na ndoa.
Sisi (na Diamond) tulikuwa Afrika Kusini, baby wangu akaipenda pete, akainunua na kunivalisha, haina uhusiano na ndoa
alisema Wema.
>>>GPL
kama
huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe
zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu.LIKE HAPA