ZAHANATI YA WAGONJWA WA EBOLA YAVAMIWA,WAGONJWA WATOROKA
http://melckstudio.blogspot.com/2014/08/zahanati-ya-wagonjwa-wa-ebola.html
Kituo
kilichotengwa na kuwekewa karantini kwa sababu ya ebola, kimeshambuliwa
na zana kuporwa katika mji mkuu wa Liberia, Monrovia.
Watu
kama 20 hadi 30 waliowekwa hapo kuangaliwa kama wana dalili za ebola
walitoroka baada ya kituo hicho kuporwa Jumamosi usiku..
Washambuliaji walipora magodoro na vitu vyengine.Kituo kiko kwenye mtaa wa West Point, wenye wakaazi wengi.
Mwandishi wa BBC katika kanda hiyo anasema pengine washambuliaji walikerwa kuwa kituo hicho kimewekwa katika mtaa wao.
Wakuu wa Liberia wanajaribu kuwatafuta wagonjwa waliotoroka ili kuwarejesha tena kwenye kituo hicho.
Watu zaidi ya 400 wamekufa kwa sababu ya ebola nchini Liberia kati ya zaidi ya 1,000 katika kanda ya Afrika Magharibi.
>>>>>BBC
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu.LIKE HAPA