MTU MMOJA AUAWA BAADA YA KUIBA BAISKELI KYELA-MBEYA


Mtu mmoja aliyefahamika kwa majina ya Lughano John aliye na miaka 36 mkazi wa Ipinda Juu ameuawa kwa kupigwa sehemu mbalimbali za mwili wake na wananchi wenye hasira kali walioamua kujichukulia sheria mkononi baada ya marehemu kutuhumiwa kuwa ameiba baiskeli.
Tukio hilo limetokea jana asubuhi ya saa nne katika kitongoji chaLutusyo, kijijini Talatala katika Tarafa ya Ntebela wilayani Kyela mkoani hapa Mbeya.
Taarifa kutoka kwa mashuhuda wa tukio zinaeleza kwamba marehemu Lughano John alikamatwa na wananchi hao akiwa na baiskeliya wizi na kisha kuanza kumshambulia kwa kumpiga hali iliyopelekea kifo chake.Wakati msako wa kuwatafuta watu waliohusika na tukio hilo ukiendelea, Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi amethibitishia Fichuo Tz kutokea kwa tikio hilo na  kutoa wito kwa wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi na badala yake wawe na tabia ya kuwapeleka watuhumiwa wanaokwamatwa katika mamlaka husika.

Related

MATUKIO 3131453594532809286

Asia - Leo

MZIWANDA - MSONDO NGOMA

TONBOY

TONBOY

CONTACT

Melck Studio
Tel : +25578920034
+255757605268
E-mail : melckstudio@gmail.com

SHOW LOVE TO THIS

Hot in week

Recent

Comments

Visitors


web stats
item