VIDEO INATISHA: KUNDI LA IS LAMKATA KICHWA MWANDISHI MWINGINE WA MAREKANI, LATISHIA KUMKATA KICHWA MWINGINE RAIA WA UINGEREZA KULIPA KISASI (ONYO VIDEO INATISHA)
http://melckstudio.blogspot.com/2014/09/video-inatisha-kundi-la-is-lamkata.html
Mwandishi aliyechinjwa na IS Steven Sotloff
Wapiganaji
wa dola ya Kiislam IS wamesambaza picha za video katika mitandao kwa
lengo la kuonyesha kuchinjwa kwa mwandishi wa habari raia Marekani
Steven Sotloff ambaye ni mmoja wa mateka wanaoshikiliwa na wapiganaji
hao.
Mwandishi huyo Sotloff, mwenye umri wa miaka 31 ambaye alitekwa na wapiganaji hao mwezi August mwaka jana.
Wapiganaji
hao wa katika picha hizo pia wameonekana wakimtishia kumuua mateka
mwingine anayedhaniwa kuwa ni raia wa Uingereza.Mwezi uliopita Sotloff
alionekana mwishoni katika picha za video zilizoonyeshwa kuhusiana na
kuchinjwa kwa mwandishi mwingine wa Marekani James Foley.
Baada ya mauaji ya mwandishi wa awali
Foley, mama mzazi wa mwandiashi wa Sotloff alitoa ombi maalumu kwa
kiongozi wa wanajeshi hao Abu Bakr al-Baghdadi kutoa muua mtoto wake.
Marekani hivi karibuni ilifanya mashambulizi ya anga dhidi ya IS nchini Iraq.
Mwandishi wa masuala ya usalama wa BBC Frank Gardner amesema hatua hiyo ya wapiganaji wa IS ni kulipa kisasi kwa Marekani.
Baada ya kukamilisha hotuba yake muuaji huyo alianza kumchinja soltloff punde tu video hiyo ilizimwa.
Sekunde
chache mateka mwingine raia wa Uingereza akaletwa DAvid Cawthorne
Haines anaonekana kabla ya Ilani kutolewa kuwa hatma yake iko mikononi
mwa taifa la Marekani.
Tazama
video hapo chini (video inatisha onyo)Video hiyo imeanza na hotuba fupi
ya Rais Obama. Baada ya hotuba hiyo, Mwandishi huyo anawekwa mbele ya
kamera na kuuawa kikatili