ASKOFU HUYU ASEMA WAGONJWA MAHUTUTI WASAIDIWE KUFA,ADAI NELSON MANDELA ALIVUNJIWA HESHIMA
http://melckstudio.blogspot.com/2014/07/askofu-huyu-asema-wagonjwa-mahututi.html
Akiandika katika jarida la ‘The Observer”,alisema yeye anasheshimu utu lakini hali inaweza kubadilika.
Pia alisema kuwa kuendeleza maisha ya Nelson Mandela ilikuwa kumvunjia heshima.
![](http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2014/07/15/140715104657_tutu_killing_512x288_bbc_nocredit.jpg)
Askofu mstaafu wa Afrika Kusini Desmond
tutu amesema kwamba anaunga mkono wagonjwa mahututi wanaotaka kusaidiwa
kufariki wafanyiwe hivyo.
Maoni ya askofu huyo mstaafu wa kanisa
la kianglikana, ni sawa na yale aliyetamka Askofu mkuu wa kanisa la
‘Canterbury Lord Carey’ ambaye pia aliunga mkono usemi huo.
Kanisa la kianglikana limeagiza uchunguzi kuhusu jambo hili.
Akiandika katika jadrida hilo, askofu
huyu mstaafu wa kanisa la Anglikana Afrikakusini na mwenye miaka
themanini na mbili alisema kwamba ”iwapo twahitaji mashine za
kupumua,bila shaka tunahitaji kuuliza ubora wake na vile fedha
zinavyotumika.”
Vile vile alieleza kuwa ni aibu vile
aliyekuwa kiongozi wa Afrika Kusini Nelson Mandela aliwekwa hai kwa mda
mrefu hospitalini katika hatua za mwisho za maisha yake huku akipigwa
picha na wanasiasa waliomtembelea.
Amesema kuwa Madiba hakujielewa kwa lolote na tendo lao lilikuwa ukiukaji wa heshima za hayati Mandela.
‘Ni kweli kwamba watu watahuzunika iwapo nitasema nisaidiwe kufa lakini kwa kauli yangu binafsi sina shaka na hilo.”
Tutu aliandika kuwa,hata ingawa
amebadilisha maoni yake,uhakika wa hapo awali hautiliwi maanani kwenye
uhalisia wa mambo yalivyo a hasa kwa wagonjwa walio mahututi.
Sheria kuhusu kusaidia wagonjwa mahututi kufariki nchini Uingereza?
Kulinganaga na sheria ya Bunge ya 1961
inayohusiana na kujiua, ni hatia kuhamasisha au kufadhili mtu kujiua
nchini Uingereza na Whales. Yeyote anayekiuka sheria hiyo huweza
kufungwa gerezani hadi miaka 14.
Sheria hii inakaribia kufanana ile iliyopo Kaskazini mwa Ireland.
![](http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2014/07/15/140715104740_mercy_killing_2_512x288_bbc_nocredit.jpg)
Nchini Scotland kuna utata kwani hakuna
sheria maalum inayohusishwa na kujiua, japo kwa maandishi na nadharia
mtu huweza kuhukumiwa chini ya sheria zinazohusishwa na kujiua.
Je, Kumekuwepo na jaribio la kubadili sheria hiyo?
Kumekuwa na majaribio kadhaa ya kuhalalisha ufadhili wa wanaotaka kusaidiwa kufariki ,lakini hakuna jitihada iliyofua dafu.
Wanaharakati waliofanya majaribio ya
kubadili sheria hiyo walibuni na kugharamia shughuli za tume
itakayoshughulikia maswala yanayohusiana na ufadhili wa wanaotka
kusaidia kufariki.
Tume hiyo ilitoa kauli kuwa mnamo mwaka
2012 kulikuwa na kesi ngumu ya kuruhusu kufadhili kifo cha wagonjwa
mahututi nchini Uingereza na Whales
Hii ni kinuyume na madai yanayotolewa na
taaluma ya matibabu, makundi ya kutetea haki za walemavu, na makundi
mengine yanayodai kuwa sheria hiyo haifai kubadilishwa ili kulinda
vikundi vilivyomo kwenye hatari ya kunyanyaswa na jamii.
Je, hali iko vipi ughaibuni?
Katika nchi zingine kama Ubelgiji,
Luxembourg na Uholanzi, sheria zimebuniwa zinazoruhusu kufadhili kifo.
Ufaransa inakadiria uwezekano wa kuanzisha sheria kama hiyo, japo kuna
upinzani mkali kutoka kwa baraza la maadili ya matibabu nchini humo.
Kundi la makampeni lifahamikalo kama
“Dignity in Dying” linatabiri kuwa huenda nchi nyinginezo zikafuata
mkondo huo wa kuhalalisha sheria hiyo.
Hata hivyo askofu mkuu wa Canterbury,
Justin Welby, anachukulia muswada huo unaohusiana na kufadhili kifo kuwa
hatari na kanisa la Uingereza linataka swala hilo kupelelezwa.
Kanisa hilo lilisema tume ya kifalme
izingatie maoni ya kitaalamu na kukadiria kwa makini madai tofauti.
Kanisa linaamini kuwa muswada uliopo sasa unafaa kutupiliwa mbali na
kutoa nafasi ili upelelezi kufanywa.
Watu 110 wanameandikishwa kuzungumza siku ya Ijumaa, muswada huo utakapojadiliwa.
Askofu mkuu Desmond Tutu ametoa mwelekeo
kuwa mjadala huo utafanyika siku ya kuadhimisha kifo cha Mandela, siku
ambayo hayati Mandela angefikisha miaka 96.
>>>>>BBC
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapowekwa kwenye mtandao huu.LIKE HAPA