CHRIS BROWN BADO ANAMZIMIKIA BABY WAKE WA ZAMANI RIHANNA
http://melckstudio.blogspot.com/2014/07/chris-brown-bado-anamzimikia-baby-wake.html
Kila mtu ana story yake ya uhusiano wake na mpenzi wake lakini hii
story ya Chris Brown na Rihanna inachukua attention ya watu wengi
kutokana na mambo yanayoendelea kati yao.
Kila muda ukipita inatokea tetesi kwamba Chris Brown ana mawasiliano
ya siri na Rihanna lakini bado hakukuwa na ushahidi kuthibitisha hilo.
Kitu kipya hivi sasa kinachotafsiriwa kwamba bado Chris ana mawazo na
kumbukumbu juu ya uhusiano wake na Rihanna ni kutokana na picha ya
rafiki wa Rihanna. Melissa Ford ambaye ni rafiki wa karibu wa Rihanna
ali post picha ya Chris na Rihanna na kuandika kuwa ni hao ndio couples
anaowapenda.
Baada ya hapo Chris Brown ali like hiyo picha na kuonyesha kwamba
amefurahia hiyo post. Kutokana na ukaribu wa Rihanna na Melissa sio
rahisi kwa Melisa ku post picha hiyo kama mambo bado ni mabaya kati ya
Riri na Chris. Kama kuna lolote linaendelea kati ya Chris Brown na
Rihanna lazima Melissa Ford awe anajua kwasababu wapo karibu sana.

Wachambuzi wanasema kwamba kuna kitu kinaendelea chini kwa chini kati
ya Chris Brown na Rihanna na hivi karibuni kinaweza kuwekwa wazi.
Rihanna na Melissa Ford
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapowekwa kwenye mtandao huu.LIKE HAPA