ETO'O ASHTAKIWA KWA KUUZA PICHA ZA NGONO NA KUUZA MALAYA
http://melckstudio.blogspot.com/2014/07/etoo-ashtakiwa-kwa-kuuza-picha-za-ngono.html

Eto’o
anaweza kuuhesabu 2014 kama mwaka mbaya kwake baada ya timu yake ya
taifa kufanya vibaya kwenye michuano ya kombe la dunia lakini pia hana
Club ya kuichezea baada ya kumaliza mkataba wake na Chelsea, kama hiyo
haitoshi kwa sasa kilichombele yake ni kesi nzito Mahakamani.
Kesi
hizo za udhalilishaji ni kutokana na kusambaza picha za utupu, vitisho,
ununuzi/uuzaji wa binadamu na udanganyifu zimefunguliwa kwenye Mahakama
moja jijini Yaounde, Cameroon ambapo aliezifungua ni aliyekuwa mchumba
wake wa zamani Hélène Nathalie Koah.
Mapema
wiki iliyopita Koah alifungua kesi hizo dhidi ya Eto’o ambaye amekana
mashtaka hayo huku hili likiwa limetokea siku chache baada ya kusambaa
kwa picha zake za utupu kwenye mtandao Facebook ambazo mhudumu huyo wa
zamani wa ndege amesema zimesambazwa na Eto’o aliyekuwa mpenzi wake.
Eto’o
amekanusha kuhusika na hilo na katika kujibu mapigo mchezaji huyo
anayeongoza kwa kutwaa tuzo nyingi za uchezaji bora barani Afrika,
amefungua kesi ya matumizi mabaya ya fedha($410,755) alizompa Ms Koah
kwa ajili ya kufungua taasisi ya kusaidia jamii wakati walipokuwa
wapenzi.

kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapowekwa kwenye mtandao huu.LIKE HAPA