MATUKIO:- BWENI LA SHULE YA SEKONDARI ERIKISONGO WILAYANI MONDULI LATEKETEA KWA MOTO LEO
http://melckstudio.blogspot.com/2014/07/matukio-bweni-la-shule-ya-sekondari.html
Kiasi
cha wanafunzi 100 wa shule ya sekondari ya Erikisongo wilayani Monduli
wamenusurika kifo baada ya vyumba vitano vya mabweni yao kuteketea na
moto leo (Jumatano) asubuhi.
Moto huo ambao inaelezwa chanzo chake ni hitilafu ya umeme ilitokea wakati wanafunzi wote wako darasani.
Hakuna
mtu yoyote aliyedhurika lakini mali kadhaa za wanafunzi zimeteketea.
Kikosi Cha zimamoto kutoka Arusha kilifika wakati tayari mabweni hayo
yameshateketea.
Mbunge
wa Jimbo la Monduli Mh Edward Lowassa ametembelea shule hiyo na
kuahidi kuwasafirisha wanafunzi majumbani kwao wakati utaratibu
unafanywa kurejesha katika hali ya kawaida.
Gharama
za kuwasafirisha wanafunzi hao ni shilingi laki Saba. Aidha Mh Lowassa
amesema kiwanda Cha magodoro Cha Tanform Cha Arusha kimetoa msaada wa
magodoro 100 kufuatia kadhia hiyo.
Kikosi Cha zimamoto kikijaribu kupambana na moto ulioteketeza mabweni ya shule ya sekondari ya Erikisongo mjini Monduli.
Mbunge wa Monduli Mh Edward Lowassa akikagua mabweni ya shule ya sekondari ya Erikisongo Monduli mjini yaliyoteketezwa kwa moto.
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapowekwa kwenye mtandao huu.LIKE HAPA