MATUKIO:-MABOMU YA MACHOZI YALAZIMIKA KUTUMIKA KUWATAWANYA WANANCHI WALIOVAMIA NA KUANZA KUCHOTA MAFUTA KWENYE LORI LA MAFUTA BAADA YA KUPATA AJALI MKOANI IRINGA





Jeshi la polisi mkoani Iringa limetumia mabomu ya machozi kuwatawanya wananchi ambao walivamia na kuanza kuchota mafuta kwenye lori la kubeba mafuta baada ya kupata ajali. 
 
Ajali hiyo imetokea jana eneo la msitu wa serikali wa Saohil wilayani Mufindi kwenye barabara kuu ya Iringa –Mbeya ambapo watu wawili walijeruhiwa kwenye ajali hiyo.
 
Polisi wamelazimika kutumia mabomu kuwatawanya wananchi hao ambao walikuwa wakiendelea kumiminika kutaka kuiba mafuta kwenye lori hilo ili kuwaepusha na hatari ambayo ingeweza kutokea kama lori hilo lingeshika moto.
 
Mashuhuda wamesema chanzo cha ajali hiyo ni kupasuka kwa tairi ya mbele ya lori la mizigo lililokuwa linatokea mkoani Mbeya na hivyo kukosa mwelekeo na kuligonga gari la kubeba mafuta lililokuwa linatokea mkoani Iringa na kuanguka.
 
Jeshi la polisi mkoani iringa limethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kwamba uchunguzi wa chanzo cha ajali hiyo unaendelea.

 kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapowekwa kwenye mtandao huu.LIKE HAPA

Related

MATUKIO 8712109098815592198

Asia - Leo

MZIWANDA - MSONDO NGOMA

TONBOY

TONBOY

CONTACT

Melck Studio
Tel : +25578920034
+255757605268
E-mail : melckstudio@gmail.com

SHOW LOVE TO THIS

Hot in week

Recent

Comments

Visitors


web stats
item