MBASHA APANDISHWA TENA MAHAKANI LEO
http://melckstudio.blogspot.com/2014/07/mbasha-apandishwa-tena-mahakani-leo.html
Katika
kesi hiyo inayoendeshwa na Hakimu Wilbert Luago,amelazimika kuhairisha
kesi hiyo kwa muda wa nusu saa kwa hoja aliyoitoa Mbasha kwamba ana
wakili wa kumtetea lakini alishindwa kufika kutokana na matatizo ya
usafiri.
Kauli
hiyo ya Mbasha ilimfanya Hakimu Luago kuhoji kama kweli alikuwa na nia
ya kuwa na wakili au ana nia ya kuweka wakili kwani tangu kesi hiyo
imeanza Mbasha hajapeleka wakili yoyote.
Mara
baada ya nusu saa kupita Wakili wa mshitakiwa alituma muakilishi wake
kuwakilisha barua za dharula ambazo zilionesha kuwa yupo safarini mkoani
Arusha na kuomba kesi hiyo kuahirishwa.
Emanuel
Mbasha ana kabiliwa na kesi mbili za ubakaji ambapo inadaiwa alitenda
makosa hayo maeneo ya Tabata katika nyakati mbili tofauti,Mbasha
alisindikizwa mahakamani na ndugu zake huku Mkewe Flora Mbasha
kutoonekana Mahakamani na badala yake alionekana mdogo wake Flora ambaye
ni shemeji yake Emanuel Mbasha.
Kesi hii imehairishwa mpaka July 23 mwaka huu.
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapowekwa kwenye mtandao huu.LIKE HAPA