MBRAZIL MWINGINE WA PILI ATUA NDANI YA WATOTO JAGWANI
http://melckstudio.blogspot.com/2014/07/mbrazil-mwingine-wa-pili-atua-ndani-ya.html
Wiki
chache baada ya kumsajili kiungo mshambuliaji wa kibrazil Andrey
Coutinho – klabu ya Yanga leo hii imefanya usajili mwingine wa mchezaji
kutoka Brazil.
Usajili
wa sasa ni wa Mshambuliaji wa kimataifa kutoka nchini Brazil Geilson
Santos Santana “Jaja” ambaye amewasili leo mchana jijini Dar es salaam
akitokea jijini Sao Paulo tayari kwa kuanza kazi ya kuitumikia klabu ya
Young Africans Sports Club kwa msimu wa 2014/2015.
Jaja
ambaye alikua akichezea timu ya Itabaina FC nchini Brazil, anakuwa ni
mchezaji wa pili kuungana na kikosi cha Young Africans baada ya Andrey
Coutinho kuwa mchezaji wa kwanza kujiunga na kikosi cha kocha Marcio
Maximo.
Usajili
wa wachezaji hawa ni muendelezo wa uongozi wa Young Africans
kuhakikisha msimu ujao unakua na kikosi bora ambacho kitaweza kufanya
vizuri kwenye michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom na mashindano ya Kombe la
Shrikisho Barani Afrika.
Jaja
anaungana na makocha wabrazil Marcio Maximo na Leonardo Neiva na kiungo
Andrey Coutinho katikaa msimu huu ambapo kwa pamoja ushirikiano wao na
wachezaji wengine wazawa wataisaidia Young Africans kufanya vizuri.
Kesho
asubuhi Jaja anatarajiwa kuanza mazoezi katika shule ya sekondari
Loyola ikiwa ni sehemu ya maandaliz ya michuano mbalimbali
itayowakabili.
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapowekwa kwenye mtandao huu.LIKE HAPA