MELI YENYE SHEHENA YA MADAWA YA KULEVYA YAKAMATWA MOMBASA
http://melckstudio.blogspot.com/2014/07/meli-yenye-shehena-ya-madawa-ya-kulevya.html
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj-QAyoGO4FqUvZ_9uoSm54GFIWZSqh28rDkucKFnAvHzOF70yIvY9ECbKSooTweYUtXco-4UaCXu8f5QEJAzaoaPZggPaazkZend5Cl0YfwragULpKlEsYiz9Kno3vjKraHZYmaiJv4jI/s640/madawa.jpg)
Maafisa
wa kiusalama jijini Mombasa wamefanikiwa kukamata shehena ya madawa ya
kulevya aina ya Heroin,mkuu wa kikosi cha kupambana na mihadarati Hamis
Masha amesema kwamba shehena hiyo lenye kilo 341.7 ambayo thamani yake
nishilingi bilioni 1.1.
Shehena
hiyo imenaswa baada ya msako wa siku kadhaa unaoendelea Kenya dhidi ya
meli ya MV Bushehr Amin Darya ambayo haijulikana imetoka nchi gani.
Kwa
sasa maafisa wakuu wanajaribu kufatilia ushahidi walio nao ili kujua
chanzo na sehemu ilikokuwa ikipelekwa mihadarati hiyo iliyo naswa Jioni
ya July 15 baada ya meli hiyo kuweka nanga bandari ya Mombasa.
Wiki
uliopita washtakiwa wawili walikamatwa baada ya kunaswa na pakiti ya
kilo moja ya dawa aina Heroin na uchunguzi ulipowafatilia zaidi
wachunguzi hao walipata kilo 341.7.kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapowekwa kwenye mtandao huu.LIKE HAPA