MKOKOTENI WA NG'OMBE WAUA MWANAFUNZI
http://melckstudio.blogspot.com/2014/07/mkokoteni-wa-ngombe-waua-mwanafunzi.html

Kamanda wa polisi mkoa wa Singida,
Geofrey Kamwela aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa ajali hiyo ni
ya juzi saa 3:00 asubuhi katika kijiji cha Uwanza wilayani Iramba.
Kamwela alisema mkokoteni huo, ambao
ulikuwa ukiongozwa na baba mlezi wa mtoto huyo, Samwel Napegwa ulikuwa
umepakia miwa kutoka kijiji cha Galanzala na ulipofika kijijini hapo
ulimgonga mwanafunzi huyo wakati akijaribu kudandia nyuma.
Alisema kuwa baada ya mwanafunzi huyo
kushindwa kudandia kikamilifu, aliteleza kisha kuingia kwenye uvungu wa
mkokoteni huo na hivyo kukanyagwa hadi kifo chake.
Kamwela alisema uchunguzi wa awali,
unaonesha kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa mwongoza mkokoteni
huo, ambaye alishindwa kumzuia mwanafunzi huyo kudandia mkokoteni.
Kamanda huyo alisema Napegwa alitoroka na kukimbilia kusikojulikana baada ya kutokea ajali hiyO