MTOTO ALIYEPOTEA AKUTWA AKIWA UCHI WA MNYAMA AMENYONG'ONYEA
http://melckstudio.blogspot.com/2014/07/mtoto-aliyepotea-akutwa-akiwa-uchi-wa.html
MTOTO
Lusia Moga (2) aliyepotea katika mazingira ya kutatanisha Julai 8,
mwaka huu kati Kijiji cha Bukore wilayani Bunda, Mara amekutwa akiwa
mtupu nyumbani kwa Magembe Nyabu, mkazi wa kijiji hicho.
Kupatikana
kwa mtoto huyo juzi alfajiri kuliibua hofu ya kuwepo kwa ushirikina
iliyotawala kwa wazazi wa mtoto huyo na wakazi wengine kijijini hapo.
Ofisa
Mtendaji wa Kijiji cha Bukore, Moshi Madeni, alisema licha ya mtoto
huyo kukutwa utupu, alikuwa amenyong’onyea kwa sababu ya njaa.
“Tulipomwona
watu walijaa kumshuhudia, lakini mama yake alikataa kumbeba hivyo mtoto
huyo alibebwa na mtu mwingine. Kitu cha kwanza alipewa uji kwa sababu
alikuwa na njaa.
“Mpaka
sasa mtoto huyo anaendelea vizuri, taarifa polisi tumepeleka na hakuna
mtu yeyote aliyekamatwa kuhusu tukio hilo,” alisema ofisa mtendaji.
via>>Tanzania Daima
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapowekwa kwenye mtandao huu. LIKE HAPA