PICHA ZA UTENGENEZAJI WA VIDEO YA PROF J NA DIAMOND Picha
http://melckstudio.blogspot.com/2014/07/picha-za-utengenezaji-wa-video-ya-prof.html
Mwanzoni
wakati zinasambaa picha za Diamond akiwa na Profesa Jay watu wengi
tulikua tukijiuliza aina ya muziki ya muziki unaotaka kufanywa na wawili
hawa ambao kwa hesabu ya haraka haraka tulishindwa kujua kama utakua
muziki wa hip hop au wakuimba kama aufanyao Diamond.
Wimbo
ulipotoka kila mtu alielewa kilichozungumzwa na Profesa Jay hasa upande
wa mashairi akitoa ushuhuda wa maisha yake ambayo yameongelewa mengi
mpaka hapo alipo kiasi cha kuuliza ‘Kipi Sijasikia’
Video
yake imeanzwa kutengenezwa July 12 ikimhusisha pia Super Producer wa
wimbo huu P.funk Majani ambaye kwa video hii kasimama kama wakili pamoja
na Diamond Platnumz upande wa pili.
Video hii inaongozwa na Adam Juma kutoka Next Level,baadhi ya vipande wakati video hii ikifanywa ni hivi.
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapowekwa kwenye mtandao huu.LIKE HAPA






























