MATOKEO YA CHANJO YA UGONJWA WA DENGUE
http://melckstudio.blogspot.com/2014/07/matokeo-ya-chanjo-ya-ugonjwa-wa-dengue.html
Utafiti
kutoka katika jarida la Lancet unaonyesha zaidi ya asilimia 50 ya
watoto ambao wamepewa chanjo hiyo wamepata ulinzi dhidi ya ugonjwa huo.
Nusu ya idadi ya watu duniani wako katika hatari ya kuambukizwa virusi vya ugonjwa huo vinavyotokana na mbu.
Wataalam
wanasema ingawa utafiti umekuwa ni wa muda mrefu wameahidi chanjo ya
ufanisi mkubwa na muhimu ili kufanikisha lengo lao.
Kwa sasa hakuna tiba ya kuzuia homa ya dengue ugonjwa ambao unaathiri zaidi ya watu milioni moja kwa mwaka.
Katika
utafiti wa awali wa chanjo hiyo, watafiti kutoka vituo vitano katika
bara la Asia waliwatibu watoto 6,000 wenye umri kati ya miaka miwili na
14.
Chanjo
hiyo pia ina manufaa katika aina nyingine za magonjwa, na inapunguza
idadi ya watu wanaohitaji matibabu katika hospitali kuanzia asilimia 80
ya kesi ya homa ya hemorajiki ambayo imekuwa ikitishia maisha ya watu.
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapowekwa kwenye mtandao huu.LIKE HAPA