YALIYOJIRI KWENYE MECHI YA JANA KOMBE KA DUNIA
http://melckstudio.blogspot.com/2014/07/yaliyojiri-kwenye-mechi-ya-jana-kombe.html
Hatimaye
michuano ya kombe la dunia inafikia tamati leo kwa mchezo wa fainali
kati ya Ujerumani dhidi ya Argentina, wakati usiku wa jana mshindi wa 3
wa michuano hiyo aliamuliwa kwa mechi kati ya Uholanzi vs Brazil.
Mchezo
huo uliopigwa kwenye uwanja wa taifa wa nchi hiyo, Brasilia, uliisha
kwa matokeo ya ushindi wa 3-0 kwa Uholanzi, kikiwa kipigo cha pili cha
Brazil ndani ya juma moja tangu walivyopokea kipigo cha magoli 7-1
kutoka Ujerumani.
Magoli ya Uholanzi yalifungwa na Van Persie, Blind na Georginio Wijnaldum.
Wakati
kocha wa Uholanzi Louis Van Gaal akielekea Manchester United, kocha wa
Brazil Luis Fellipe Scorali amesema pamoja na kuvurunda kwa Timu yake
lakini hawezi kujiuzulu na hatma yake anaiacha mikononi mwa waajiri wake
shirikisho la soka la Brazil.
